KIONGOZI MKUBWA KUZINDUA HOSPITALI NA OFISI NDOGO YA MAGEREZA

Na  Mwandishi wetu, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, George Simbachawene ameahirisha uzinduzi wa jengo la hospitali ya magereza na ofisi ya ndogo ya Makao Makuu ya Magereza mkoa wa Dar es Salaam na kuahidi atakayezindua atakuwa ni kiongozi mkubwa. 


Hayo ameyasema baada ya kumaliza kufanya ukaguzi wa majengo hayo pamoja na fremu za biashara zilizojengwa na jeshi la Magereza, eneo la Ukonga  jijini Dar es Salaam leo.


Amesema  kwa kazi kubwa waliyoifanya magereza anatamani atafute mtu mkubwa wa kuzindua majengo hayo. 


"Jeshi la sasa chini ya uongozi wa Rais Dk John Magufuli linasimama kwa haraka na kufanya kazi kwa muda mchache."

Kwa kazi mliyoifanya nawapongeza  lakini tambueni leo nimekuja kukagua lakini kuna mabadiliko ambayo atakayekuja kuzindua atakuwa mtu mkubwa nami nitahusika kuisoma risala." Amesema. 


Amesema kwa mfano jengo la ofisi ya mkuu wa Magereza Dar ea Salaam likianza kujengwa mwaka 1992 na kutelekezwa ambapo hadi sasa nia miaka 28. 


Simbachawene amesema  kwa mradi wa hospitali umefikia robo na jengo la wagonjwa wa nje limeshakamilika huku mengine yakiendelea kukamilika. 


"Najua tamanio la Rais Dk. Magufuli ni kuona jeshi la Magereza limefikia hatua ya kujitegemea hivyo nimeamua muendelee kumalizia maemeo ambayo bado na mimi nimuombe kiongozi mkubwa aje kuyazindua, "amesema. 


Almefafanua dhama ya magereza ni kuwepo na watu wa kujitegemea  ili kuyafikia maendeleo na mimi sipo tayari kuona jeshi legelege na la kikoloni bali linalozalisha na kupambana na changamoto. 


"Ninasema hivyo kwa sababu ardhi mliyonayo  ni kubwa na ikitumika vizuri italeta mafanikio makubwa. 


"Sasa majengo yanayotarajia kumalizika malizieni hasa wodi ya wazazi na ukiiunganisha na OPD ndipo itajulikana kinachozinduliwa ni hospitali,  zahanati au kituo cha afya ambayo itatoa huduma kwa wananchi,  "amesema. 


Pia amewaasa kuzingatia sheria na kanuni ili kazi zifanyike kwa uzuri. 


Hata hivyo Mkuu wa Magereza mkoa wa Dar es Salaam, George Wambura amesema watahakikisha wanatumia muda zaidi ili kukamilisha.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, George Simbachawene akizungumza wakati akihairisha kufungua jengo la ofisi na hospitali ya Magereza iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar Es Salaam, George Wambura akizungumza jijini Dar es Salaam leo akisema kuwa watahakikisha wanatumia muda zaidi ili kukamilisha.

Baadi ya maafisa magereza wakiwa katika uzinduzi wa jengo la ofisi pamoja na Hospitali ya Magereza iliyopo ukonga jijini Dar es Salaam.

x

No comments: