JOWUTA yawatunukia wanahabari wa Njombe Vyeti
Na Amiri Kilagalila,Njombe
Zaidi ya waandishi wa habari 17 wawakilishi kutoka vyombo mbali mbali Tanzania mkoani Njombe,wametunukiwa vyeti vya ushiriki wa semina na mafunzo ya Jinsia na usalama mahala pa kazi kutoka Chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA)
Wanahabari hao wametunukiwa vyeti vya ushiriki mara baada ya kuhitimisha semina ya siku mbili iliyofanyika katika ukumbi wa Dosmeza mjini Njombe huku wakitakiwa kwenda kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi huku wakizingatia maadili ya kazi zao.
No comments: