IGHONDO: CHAGUENI VIONGOZI WATAKAO WAPA MAJIBU YA CHANGAMOTO ZENU


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhani Ighondo,  akihutubia kwenye mikutano ya kampeni alioifanya katika Kata ya Mughunga na Mgori katika jimbo hilo juzi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhani Ighondo, akiwasili Kata ya Mgori kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kampeni.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhani Ighondo (kulia) akiwa na Mgombea Udiwani wa Kata ya Mgori, Zuma Abdallah.  
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo 
( CHADEMA) Wilaya Singida, Jimbo la Singida Kaskazini  Frank Petro ambaye baadae alijiunga na CCM, akimuombea kura, Rais John Magufuli, Mbunge Ramadhani Ighongo na mgombea udiwani wa Kata ya Mgori, Zuma Abdallah kwenye mkutano huo,
Meneja Msaidizi wa  kampeni wa mgombea huyo, Shabani Limu, akihutubia kwenye mkutano huo.
Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Mkoa wa Singida, Pascal Nzuri, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Denis Nyiraha, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mgombea udiwani wa Kata ya Msange,  Eliya Digha akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Mradi wa Ufugaji Nyuki na Uhifadhi wa Mazingira Wilaya ya Singida, Rajabu Mumbee, akizungumza katika mkutano huo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhani Ighondo (kulia) akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Mgori, Zuma Abdallah. 


 

Na Dotto Mwaibale, Singida.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhani Ighondo amewahimiza wananchi kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo.

Ighondo alitoa ombi hilo juzi wakati akihutubia kwenye mikutano ya kampeni alioifanya katika Kata ya Mughunga na Mgori katika jimbo hilo.

" Ndugu zangu ifikapo Oktoba 28 msifanye msaha nendeni mkawachague viongozi kutoka CCM ambao ndio wenye uwezo wa kuwaleteeni maendeleo na kuwapa majibu ya changamoto zenu na sio hao wengine ambao wanaibuka wakati wa uchaguzi tu" alisema Ighondo.

Ighondo alisema uchaguzi sio lelemama kwani wakikosea na kuwachagua  viongozi wasiofaa wajue watakosa maendeleo kwa miaka mitano hivyo aliendelea kuwasihi wananchi hao kuchagua viongozi ambao watakuwa na tija kwao.

Ighondo alisema iwapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa ataunda vikundi vya wajasiriamali ili waondokane na umaskini na kuwa ataongeza nguvu kwa umoja wa wana Singida Kaskazini ambao wapo nje ya mkoa na nje ya nchi ambao una mizinga 50  kwa ajili ya ufugaji nyuki katika Kijiji cha Ngimu.

Mgombea udiwani wa Kata ya Msange,  Eliya Digha akizungumza kwenye mkutano huo alizitaja baadhi ya  changamoto zinazowakabili wananchi wa Mgori kuwa ni kukamilisha ujenzi wa baadhi ya madaraja ili kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi wakati wa mvua ambapo alimuomba Ighonda iwapo atachaguliwa kulifanyia kazi jambo hilo.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa  kampeni wa mgombea huyo, Shabani Limu alisema kuwa vyama vya upinzani wasitegemee kupata nafasi katika jimbo hasa kutokana na kazi nzuri aliyoifanya Rais John Magufuli ya kuwapelekea maendeleo katika jimbo hilo na Tanzania kwa ujumla.

" Niwahakikishie wapinzani kuwa kwa kazi kubwa ya maendeleo aliyoifanya Rais Magufuli wasitegemee kupata hata jimbo moja" alisema Limu.

Mgombea Udiwani wa Kata hiyo ya Mgori, Zuma Abdallah alisema iwapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa atashirikiana na mbunge na kuhakikisha wananchi wao wanapata maendeleo na kuondokana na  changamoto mbalimbali walizo nazo

No comments: