CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUFUNGUA TAWI LAO DODOMA IKIWA NI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUHAMIA MAKAO MAKUU
Charles James, Michuzi TV
CHUO cha Uhasibu Arusha (The Instistute of Accontancy Arusha IAA) ambacho kipo chini ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kinatarajia kufungua tawi (Campas) la Chuo hicho katika Mkoa wa Dodoma lengo likiwa kuunga Mkoano Jitihada za Serikali katika Sekta ya Elimu .
Akizungumza leo na wandishi wa habari jijini Dodoma Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamini Sedokeya amesema ili kuweza kuendana na jitihada za serikali wameona ni vyema kama chuo wakatoa mchango wao katika kuhakikisha kwamba wanaongeza tawi (Campas).
‘’ Kuzingatia kuwa nchi imehamia katika Makao Makuu ya nchi yamehamia Dodoma kwahiyo sisi kama chuo tukasema na sisi ni wajibu na niwakati muafaka wa sisi kwenda Dodoma ‘’
Amesema toka awamu ya tano ilivyoingia madarakani kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya Elimu kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jonh Pombe Magfuli alikuja na mpango wa kutoa Elimu bure kwamaana ya Elimu bila malipo katika ngazi za msingi na sekondari hivyo hiyo imepelekea mahitaji katika vyuo kuongezeka sana
‘’ kwahiyo unaona ongezeko hilo wote labda hawataweza kwenda high school lakini vile vile wakija vyuoni masalani inawezekana tusiweze kuwapokea wote kwahiyo ili kuendana na jitihada za serikali tukaona kama chuo tutoe mchango wetu kuhakikisha kwamba tunakua.’’
Profesa Sedoyeke amesema mpaka sasa wametafuta katika la eneo Njendengwa wamelilipia ambapo kwa sasa wapo katika hatua za mwisho kwaajili ya kupata hati na tayari michoro na taratibu nyingine za ndani za kibali kwaajili ya kuanza kujenga zimekwisha kuanza.
‘’ Kwa hiyo sasahivi kufungua tawi (Campas) Dodoma ni kitu ambacho kipo tayari kwenye mwendo na tunategemea mwakani tukawa na tawi (Campas) ambayo iko kamili inayotoa kozi zote kuanzia ngazi ya cheti mpaka Masters’’ Amesema Prof Sedoyeke.
Amesema mpaka sasa wanakozi hamsini (50) huku wakijiendesha katika Matawi makubwa matatu ikiwemo Arusha,Babati na Dar es salaam.
‘’mpaka sasa tunawanafunzi takribani elfu tano tukiwa na waajiriwa kama mia mbili ishirini vile vile chuo kimeendelea kushirikiana na taasisi mbalimali kama jeshi ,"
Chuo cha uhasibu Arusha ni chuo cha Serikali kilicho anzishwa miaka ya themanini kama kituo cha kutengeneza wataalamu wa uhasibu baada ya hapo serikali iliona umuhimu wa kuwa chuo kamili ,sheria ya Namba moja (1) 1990 ikaanzisha chuo rasmi ambapo kwa sasa wanakwenda miaka thelathini ya chuo hicho .
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha IAA akifafanua jambo kwa wandishi wa habari jijini Dodoma alipokua akitangaza azma ya Chuo hicho kufungua tawi lake jijini Dodoma ukiwa ni mpango wao wa kuunga mkono juhudi za serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi jijini Dodoma.
No comments: