WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AWAASA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KULIOMBEA TAIFA
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amewaasa viongozi wa Dini nchini kuendelea kuliombea Taifa hasa tunapoelekea katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu ili nchi iendelee kuwa na amani na utulivu.
Akizungumza leo mara baada ya kufungua mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos limited ya jijini Dodoma Pinda amesema,bado kuna haja kwa viongozi wa dini kuombea kampeni iwe na amani na utulivu lakini pia zifanywe kwa misingi ya kuheshimia baina ya mgombea na mgombea.
"Viongozi wa dini waendele na moyo wa kuliombea Taifa ili kampeni ziende vizuri,na kila mmoja katika jamii atambue amani na utulivu ni mambo ya msingi sana." Amesema Pinda.
Awali akifungua mkutano huo kiongozi huyo amewataka wanachama wa Sacco's hiyo kutumia mikopo kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla na siyo vinginevyo.
Pinda ambaye ambaye pia ni manachama wa Sacco's hiyo amesema,uwepo wa Sacco's nchini umesaidia wananchi kujiongeza na kufanya shughuli za kujiongezea kupato lakini pia zimetoa ajira.
Amesema kutoka mwaka 2015 Sacco's zimeongezeka kutoka 4,206 hadi 6,178 mwaka huu lakini pia idadi ya wananchi waliojiunga na Sacco's mbalimbali nchini ineongezeka katika kipindi hicho kutoka 676,202 hadi kufikia milioni 2.4.
Aidha amesema ,mitaji,amana,akiba na hisa navyo vimeongeze kutoka shilingi bilioni 428.8 hadi kufikia shilingi bilioni 819.
"Mchango wa Sacco's siyo mdogo,ni chombo sahihi kinachoweza kuifikisha nchi mahali pazuri,pia Sacco's zina nafasi kubwa na masharti nafuu tofauti na benki,tuzitumie ." amesisitiza.
Amewataka wanachama wa Sacco's hiyo kukipa na kulipa kwa wakati ili wanachama wote wapate fursa ya kukopa .
Mapema Mwenyekiti wa Bodi wa Sacco's hiyo Ibrahim Sumbe amesema Sacco's hiyo ilianza mwaka 2004 ikiwa na wanachama 89 ambapo hadi kufikia Agosti mwaka huu kuna wanachama 653 .
Pia amesema Sacco's hiyo ilianza na fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.7 ambapo hadi Agosti mwaka huu ina shilingi bilioni 600.4 huku akisema madhumuni ya kuanzishwa Sacco's hiyo ni kujiinua kiuchumi huku akieleza mikakati yao kuwa ni pamoja na kupanua huduma za kifedha na kujenga mtaji wa uhakika na kuendelea kujiinua kiuchumi .
Sumbe amesema yangu kuanzishwa kwake,Sacco's hiyo imeshatoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 14 lakini pia imetoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wake 172.
Kuhusu uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu Sumbe amesema,nchi inahitaji viongozi sahihi watakaolipeleka Taifa mbele kutoka kwenye uchumi wa Kati na kufikia uchumi wa kati ulioimarika.
"Ushirika unahitaji umoja ,amani na utulivu bila hivyo hakuna Ushirika,nchi yetu imeingia katika uchumi wa kati ,tunahitaji uongozi ambao utaendelea kutuvusha zaidi kutoka hapa tulipo." Amesema
Sacco's hiyo pia imetoa vitu mbalimbali vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni tano kwa vituo vya kulea wazee na watoto yatima pamoja na mashuka 200 kwa ajili ya hospitali ya mkoa wa Dodoma (General).
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza kwenye mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos Limited jijini Dodoma.Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Usharika wa Dodoma akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa KKKT Arusha Road Saccos leo jijini Dodoma.
Wanachama wa Saccos ya KKKT Arusha Road wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye mkutano wao ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.
No comments: