Watumishi Mloganzila wafuzu mafunzo ya mbinu za utafiti
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Julieth Magandi akiwakabidhi vyeti wahimu wa mafunzo ya mbinu za utafiti.Dkt. Julieth Magandi akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Faraja Chiwanga akifunga mafunzo ya mbinu za utafiti yaliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
Method Kazaura kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili- MUHAS- akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wawezeshaji wa mafunzo hayo. Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Muhimbili-Mloganzila Sis. Redemptha Matindi akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo ya mbinu za utafiti mara baada ya kuhitimishwa mapema hii leo.
*************************************************
Watumishi katika sekta ya afya wasisitizwa umuhimu wa kufanya tafiti katika maeneo yao ya kazi ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Faraja Chiwanga wakati akihitimisha mafunzo ya siku tano ya mbinu za utafiti yaliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Prof. Lawrence Museru, Dkt. Chiwanga amesema wataalamu wa sekta ya afya hawanabudi kujikita katika kufanya tatifi ili kuboresha njia mbalimbali za kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.
“Tukijike katika kufanya tatifi ili kuleta mapinduzi katika sekta ya afya, hivyo tutumie mafunzo haya kwa vitendo kwa kuandika tafiti mbalimbali kwa maslahi ya taifa letu” amesema Dkt. Chiwanga.
Jumla ya washiriki 25 wa kada mbalimbali wamehitimu hayo yaliyotolewa na wataalamu wabobezi katika tafiti za afya kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili- MUHAS- kwa kuratibiwa na Kitengo cha Elimu, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu MNH-Mloganzila.
No comments: