WAPEWA MAFUNZO YA TEKNOLOJIA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA JAMII.

Na Jusline Marco-Arusha

Taasisi ya Kuza Africa na kituo cha kuwaendeleza vijana na uongozi(CENTER FOR YOUTH EMPOWERMENT AND LEADESHIP) kwa udhamini wa Locolization Lab, Facebook, ICANN na AFRINIC kwa pamoja wametoa mafunzo kwa wanawake ya uelewa wa teknolojia kwa maendeleo endelevu ya jamii.

Mhadhiri wa masomo ya Teknolojia kutoka chuo kikuu cha mzumbe Dkt.Tupokigwe Isayah katika semina ya mafunzo hayo ambayo yameendeshwa na shule ya wanawake Arusha ya utawala wa mtandao kwa wanawake kutoka asasi mbalimbali za kiraia ,walemavu, wanasheria pamoja na waandishi wa habari.

Dkt.Tupokigwe alisema kuwa ushiriki wa wanawake katika utengenezaji na uboreshaji wa  teknolojia ni muhumu  kwani utawezesha  teknolojia hizo kukidhi mahitaji yao ambapo ameeleza kuwa wanawake ambao ndiyo watumiaji wa teknolojia iliyoboresha wanatakiwa kuangalia na kujaribu kuelewa mchakato mzima kwanzia kifaa kinapoanza kufanya kazi, hatua zilizotumika.

Aidha alisema kuwa lengo la semina hiyo ya mafunzo kwa wanawake ni kutoa maoni  na uelewa wa teknolojia ili kuweza kuwa na uhakika wa teknolojia iliyoboreshwa na inayotumika katika jamii kwa maedeleo endelevu ambapo pamoja na kuhakikisha kuwa teknolojia inakidhi mahitaji pia itasaidia kuleta matumizi ya vifaa mbalimbali vya teknolojia ambazo zimetelekezwa mitaani kutokana na kutokujua matumizi sahihi.

Aliongeza kuwa ipo inayosemekana kuwa sehemu ya utengenezaji wa teknolojia ni jukumu la watu wachahe lakini wanapaswa kufahamu kuwa jambo hilo kihualisia ni hatua ambayo kila mtu anatakiwa kuchukua kwani teknolojia hiyo inapaswa kuendelezwa ili kuweze kukidhi mahitaji ya watu mbalimbali.

Naye mwanzilishi wa Kampuni ya Serensic Afrika inayojishulisha na masuala usalama kwenye mtandao Esther Mengi alisema kuwa ili kuhakikisha usalama wa mtu mtandaoni unakuwepo pindi ujumbe unapotuma na kupokea majibu kabla ya kufanya  jambo lolote mtu anapaswa kuhakikisha ujumbe huo umetoka kwa muhusika na hauna kitu cha tofauti.

"Nimefurahi kuona wanawake wengi katika mfumo wa teknolojia wanafanya mambo makubwa na yatofauti,semina hii imetupa nafasi ya kuelezana  changamoto zinazowakabili wanawake katika teknolojia na tumeweza kujua ni kwanini mtu awe salama akiwa mtandaoni" alieleza Esther

Aliongeza kuwa ni lazima mtu alinde taarifa zake kwani mtu anaweza kutumia taarifa hizo zilizopo katika mitandao ya kijamii na kutengeneza akaunti bandia kwa kufanya uhalifu ikiwemo kutapeli, kupotosha jamii  na mambo mengine hivyo ameshauri matumizi ya nywila imara(password)katika akaunti za kwenye mitandao ili mtu mwingine asiweze kuingia na kujibu au kutuma ujumbe kwa watu wa muhimu na wakati mwingine kuweza kuwaharibia kazi .

Vilevile alieleza kuwa usalama wa mtandao wakati vyama vinapofanya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu  ni muhumu kwani kipindi hiki tayari ipo mifumo mingi ikidukuliwa kutokana na kunaona watu wamekuwa wakifuatilia kinachoendelea na wahalifu hao wanatumia nafasi hiyo kufanya uhalifu wa kimtandao hivyo ni vyema kuwa makini.

Sambamba na hayo  pia alizungumzia changamoto  ya walemavu wa kuona katika teknolojia zilizopo kwenye tasisi za fedha ambapo baadhi ya walemavu hao wanapenda kutoa fedha wanashindwa huku wakati mwingine wakilazimika kwenda na msaidizi kutoka na mifumo iliyopo utokuwa rafiki kwao hivyo taasisi za kofedha zina wajibu wa kuboresha teknolojia hiyo ili watu wenye walemavu hususani kwa kuona  kuweze kupata  huduma hiyo kwa urahisi  na haraka.

Kwa upande wake mwalimu wa watu wenye ulemavu wa kusikia kutoka shule ya msingi Ilboru,Linda Malisa wakati akitafsiri lugha za alama katika semina hiyo alisema kuwa matumizi ya mtandao yamewarahisishia walemavu  kuwasiliana japo kuna baadhi ya vifaa bado siyo rafiki kwa walemavu wa kuona kutokana na kutokuwa kwa maneno ya nukta nundu.

Peter Mbando ambaye ni mmoja wa waandaji katika semina hiyo alisema kuwa dhumuni la mafunzo hayo kwa wanawake ni ili kuwasaidia kuwapa elimu katika kipindi cha digitali ya mtandao kwani hivi sasa vitu vingi vinaendeshwa kwa njia ya mtandao .
 Baadhi ya washiriki waliohudhuria semina ya utawala wa mtandao iliyofanyika jijini Arusha iliyojumuisha wanahabari,asasi za kiraia pamoja na sekta mbalimbali za masuala ya sheria
 Pichani ni Mhadhiri wa masomo ya Teknolojia kutoka chuo kikuu cha mzumbe Dkt.Tupokigwe Isayah akiwasilisha mada katika semina ya wananwake ya utawala wa mtandao na umuhimu wa mwanamke kushiriki katika utengenezaji wa teknolojia iliyofanyika jijini Arusha.

No comments: