WANANCHI WA MASASI MJINI WANAHITAJI MAENDELEO KWA SASA NA SI VINGINEVYO -MWAMBE.


Na Mwandishi Wetu

Mgombea ubunge wa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM) katika Jimbo la Masasi Mjini, lililopo Mkoani Mtwara,Geoffrey Mwambe amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu ili aweze kuliongoza jimbo hilo na kuwaletea maendeleo.

Mwambe ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji(TIC) alisema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Napupa ambapo pamoja na mambo mengine, alisema kuwa, wananchi wa Masasi Mjini wanahitaji kiongozi bora atakayeweza kuwaletea maendeleo wananchi.

Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, ana kila sababu ya kuhakikisha kuwa, anagombea nafasi ya ubunge ili aweze kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wanaletaaendeleo.

"Wananchi wa Masasi Mjini wanahitaji kupata maendeleo ya kweli kupitia rasilimali wanazozalisha, ikiwamo kilimo cha mazao ya korosho, ufuta, choroko na mbaazi, hivyo basi ikiwa watapata masoko ya uhakika wanaweza kuuza mazao yao na kupata fedha ambazo zitawasaidia kupata maendeleo," alisema Mwambe.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, atahakikisha anashirikiana na serikali ili waweze kutafuta masoko ya uhakika ambayo yatawasaidia kuuza mazao yao na kupata faida.

Alisema lakini pia, atahakikisha anaboresha  miundombinu ya barabafa ili wakulima waweze kurahisisha usafirishaji wa mazao yao.

No comments: