Wanahabari watakiwa kutumia kalamu zao kuelimisha jamii

Na Woinde Shizza, Michuzi Tv ARUSHA
WANAHABARI wametakiwa kutumia kalamu zao katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa ulaji wa mbogamboga kwa ajili ya uboreshaji wa afya zao ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika nchi na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hitimisho la semina ya waandishi wa habari iliyofanyika Tengeru jijini Arusha Mkurugenzi wa world vegetable centre Gabriel Rugalema alisema kuwa waandishi ndio watu muhimu katika kufikisha habari kwa haraka zaidi kwani wameonekana ni watafiti katika mambo mbalimbali ya kijamii. 

Rugalema alisema sifa za mwandishi bora ni yule ambaye ataandika habari zenye weledi kwa kudodosa na kuchambua kwa umakini habari hiyo kwa sababu unaweza ukapewa habari ambayo haijakamilika na kutokuaminika.

"Kutokana na warsha hii mtaongeza ubora wa kazi zenu Katika kuandika habari za mada na tasnia ya mboga mboga kwani mwandishi bora anasifa ya kuwa mtafiti, mchambuzi, mtashi na mwepesi wa kujifunza, sifa hizi zinatufaa sana katika sekta ya mbogamboga alisema mkurugenzi huyo". Alisema Rugalema

 Masunga na Hilda Kinabo ni baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo walisema bado tanzania kuna ukuaji mdogo wa kilimo hicho tofauti na mataifa mengine ikiwemo ulaji wa mboga mboga huku ikiwalazimu kutoa elimu kwa jamii na umuhimu wa kilimo hicho.

Aidha wamelishukuru shirika hilo kwa kutoa mafunzo hayo kwa kuwaelimisha wakulima kutoka kwenye kilimo cha kizamani na kuingia cha kisasa na kujifunza teknolojia ya udongo kwa ajili ya kuoteshea miche kwani ni wakati wa wakulima kuamka na kuja kujifunza katika kituo hiki.

"Tumejifunza kilimo cha kimkataba ambacho kina faida kubwa kufanya mkulima anaingia shambani akiwa tayari amelifahamu soko sasa ni muda wa kutoa elimu kwa wakulima alisema kinabo". Alisema Rugalema
Mkurugenzi wa world vegetable centre Gabriel Rugalema akuonyesha waandishi wa habari namna ya kuzuia wadudu washambuliao mazao kwa kutumia mifuko ya lailoni.
mkulima wa vitunguu ambaye pia Ni mkulima anaezalisha Miche ya aina mbalimbali ya mbogamboga Alfred Lukumay akionyesha waandishi wa habari vitunguu alivyovilima Mara baada ya kupewa elimu ya kilimo Cha mbogamboga na shirika la World Vegetables center lililopo Tengeru mkoani Arusha juzi.

No comments: