Wanafunzi wa Watanzania kushindania kuiwakilisha Afrika katika mashindano ya kimataifa ya TEHAMA ya Huawei.


Johannesburg, South Africa, Septemba 13, 2020

Wanafunzi wa Tanzania ni miongoni mwa washiriki wa fainali za Mashindano ya kimataifa ya TEHAMA kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara yanayoandaliwa na Huawei chini ya kaulimbiu ya "Connectivity, Glory, Future".

Kwa mwaka jana wanafunzi kutoka Tanzania na Nigeria walikuwa washindi wa jumla katika shindano hilo na hivyo kuwakailisha ukanda huo katika mashindano ya dunia.

Shindano hilo limezinduliwa jijini Johannesburg, South Africa jana Septemba 10 katika hafla iliyofanyika kwa njia ya mtandao. Shindano hilo linaaminika kuwa ndiyo kubwa zaidi la aina yake barani Afrika kwa kushirikisha nchi 14 na kuhushisha wanafunzi zaidi ya 50,000.

Shindano la TEHAMA linaloandaliwa na Huawei, kwa mwaka huu limeshirikisha zaidi ya nchi 70 Ulimwenguni kote, na kushindanisha wanafunzi 150,000 kutoka vyuo zaidi ya 2000.

Tangu kuzinduliwa kwake miaka mitano iliyopita, Shindano la TEHAMA la Huawei limeendelea kukua na kuwa shindano kubwa Zaidi la TEHAMA barani Africa.

Katika uzinduzi uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano, UNESCO pamoja na wanafunzi, Makamu Rais wa Huawei Afrika Kusini, Ndg. Liao Yong alielezea umuhimu wa mawasiliano katika zama hizi za kutokusogeleana.

“Utofauti katika mapokeo ya kidigitali unazidi kuongezeka katika kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na janga la Covid-19. Wakati watu wanapojisomea na kufanya kazi mtandaoni, wale wenye changamoto za kidigitali wanaathirika zaidi”. Alisema Liao.

Katika semina ya mtandaoni iliyoandaliwa na UNESCO buni hivi kari,ilibainishwa kuwa miundombinu ya kidigitali ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili sekta ya elimu ya juu barani Afrika.

“Kufanya shindano hili la TEHAMA mtandaoni kwa kipindi hiki kuna thamani ya kipekee, inaonyesha kwamba Huawei kama waasisi wa miundombinu ya kidigitali Afrika pia tuko makini sana na mkakati wetu wa kuwekeza kwenye vipaji. Mkakati unajumuisha mambo matatu; kuwafundisha wataalamu wa TEHAMA kidigitali, kuhamasisha na kuwawezesha wanafunzi wa TEHAMA na kuongeza uelewa wa TEHAMA kwa watu wa kawaida.

Kampuni ya Huawei imewekeza zaidi katika kujiandaa na mashindano hayo kwa kufanya maonyesho kwenye vyuo 300, katika nchi 14 za Kusini mwa Jangwa la Sahara, na jumla ya wanafunzi 50,000 watashiriki. Mafunzo kuhusu mashindano haya yamesaidia zaidi ya wanafunzi 300 kupata ofa za kazi.

Aidha, mafunzo haya yamekuwa na umuhimu mkubwa kwa wanafunzi. Mwanafunzi wa TEHAMA wa Tanzania Emanuel Chaula alifurahi sana kwamba timu ya Wanafunzi wa Tanzania ilikuwa moja timu kutoka nchi mbili zilizoshinda katika mashindano ya mwaka jana.

"Tulifanya kazi kwa bidii kama timu kwa sababu tulitaka kutumia fursa hiyo kusafiri kwenda China kushindana katika fainali za ulimwengu mzima. Tulitaka kuonyesha Afrika na ulimwengu kuwa Tanzania ni mdau mkubwa wa TEHAMA na tunataka kuwa sehemu ya ukuaji huo katika nchi yetu.” Alisema.

Akiongea pia wakati wa hafla ya ufunguzi, Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Kimataifa ya Elimu ya UNESCO, Ydo Yao, aliipongeza Huawei kwa kuchukua jukumu la mfano kuunga mkono mipango inayounda, kubuni na kutoa ustadi wa TEHAMA kwa bara la Afrika.

Barani Afrika, ushirikiano kati ya UNESCO na Huawei umekuwa na matunda na miradi mingi iliyofanikiwa, kama DigiTruck na Akademi ya TEHAMA ya Huawei chini ya usimamizi wa mpango wa ujumuishaji wa digitali wa Huawei TECH4ALL.

Pamoja na kampeni kadhaa za mfumo wa ikolojia ya vipaji Kusini mwa Jangwa la Sahara, yakiwemo mashindano ya TEHAMA, Huawei inatarajia kufundisha zaidi ya wataalamu 700,000 wa TEHAMA ifikapo 2023. Lengo ni kuziba pengo la ujuzi wa TEHAMA, kuendeleza mabadiliko ya kidigitali kwa viwanda, na kuileta digitali kwa kila mtu, nyumba na shirika kwa ulimwengu uliounganishwa kikamilifu na wenye utaalamu zaidi.

No comments: