USHAURI WA DK. MAGUFULI KWA WAKULIMA KUHUSU MAZAO WALIYOYAPATA
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Sengerema
WANANCHI wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kutunza mazao ambayo wameyapata na wala wasiyauze vibaya.
Akizungumza na wananchi wa Senggerema Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amesema kwamba anafahamu Sengerema ni wakulima wazuri lakini amewaomba mazao wasiyauze vibaya.
”Dunia imekumbwa na Corona wakati wa Corona nchi nyingi ziliwafungia watu wake ndani(Lockdown) na hivyo watu waliokuwa wamefungiwa ndani katika nchi hizo hawakufanya chochote, wana njaa.Nchi inayotogemewa ni Tanzania, haikuwa na lock down wala mjomba wake lock down.
”Tuliomba tatizo la Corona liondoke Tanzania na kwa mapenzi ya Mungu alisikia maombi yetu.Sengerema mmepata mazao mengi, tusiwe na tamaa ya kuyauza haraka haraka, tuuze mazao yetu wakati tumepata mazao mengine, na mkiuza msiuze kwa bei ya chini.Wameanza kupita watu kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kununua mazao,hivyo lazima tutunze chakula ili baadae tusipate njaa,”amesema Dk.Magufuli.
Wakati huo huo Dk.Magufuli amesema nchi yetu hivi sasa inaonewa wivu.”Nchi yetu ilikuwa inahesabika nchi masikini leo, iko uchumi wa kati , niwaombe wana Sengerema tushikamane, hata kuwa na anamani na usalama sio kitu kidogo, hata huu Uchaguzi Mkuu mwaka huu tumetenga bajeti ya Sh.bilioni 330 ambazo zimetolewa na Serikali yetu.Hii ni kwa mara ya kwanza, huko ndiko kujitawala.”

No comments: