UJENZI WA VYOO VYA KISASA SHULE YA MSINGI MTWARA VIJIJINI WAKAMILIKA

Na ANNE ROBI Mtwara

UJENZI wa vyoo vya kisasa katika shule za msingi Wilaya ya Mtwara Vijijini umekamilika kwa aslimia 95, Mkurungezi Mtendaji wa Manispaa ya Mtwara DC Erica Yegella amesema.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo ambao unatekelezwa katika shule za msingi saba wilayani humo, Yegella amesema vyoo hivyo vya kisasa vinajegwa kupitia programu ya Afya na Elimu Shulen SWASH) umegharim kiasi cha shilingi  milioni 175.5/.

“Huu ni mradi wa bank ya dunia lakini chini ya usimamizi wa ofisi ya Raisi, Tawala za Mikoa na Serikal za mitaa TAMISEMI),” alisema mradi huo unatekelezwa katika shule saba ambazo zilikuwa na changamoto ya vyoo kwa wanafunzi pamoja na walimu.

Amezitaja shule hizo kuwa ni Libobe, Msangamkuu, Mnete, Mkonye, Nakada, Kitere na Miuta shule za msingi katika wilaya ya Mtwara vijijini

Mkurungezi huyu amesema ujenzi wa vyoo vimekamilika katika shule nne na kwamba wanafunzi wataanza kuvitumia mhula huu. “Ujenzi wa vyoo umekamilika katika shule nne bado shule tatu ambapo mafunid wako katika hatua ya ‘finishing’ ili  kukamilisha na watoto waanze kuvitumia hivyo vyoo,” amesema.

Amesema ujenzi wa vyoo hivyo umechangiwa na wananchi wa maeneo husika huku akiwashukuru kwa kujitoa katika kushiriki na kuhakikisha vyoo hivyo vinakamilika huku vingine vikifikia hatua za mwisho.

“Nawashukuru sana wananchi---wamejitoa san asana kupitia viongozi wa serikali za mitaa,” amesema na kuongeza kuwa mradi huo wa ujenzi wa vyoo pia umeleta fursa kubwa kwa wanavijiji kupitia kwa kuwapa ajira  na vibarua vya ujenzi wa mradi huo.

Amesema serikali bado ina mpango wa kutekeleza miradi mingi ya ujenzi wa madarasa pamoja na maji hivyo kuwataka wananchi kujitolea lakin pia kukusanya kokote, mawe pamoja na mchanga na kuuizua serikali kwa ajili ya kujenga miradi hiyo.

“Bado tuna mpango wa kujenga miradi mingine kama vile madarasa katika baadhi ya shule zenye uhitaji na katika ofisi yangu tunazo milioni 57/ kwa ajili ya kujenga madara,” amesema.

Kwa hatua nyingine, Yegella amewaomba wananchi wa Mtwara na wadau wengine wa maendelea kuchangia katika ujenzi wa miundombinu ya shule kwa kuchangia mabati, misumari, tofali na vifaa vingine ili kusaidia katika kujenga mazingira mazuri ya wanafunzi vijijini kusoma.

Akizungumzia changamoto zinazozikabili maendeleo ya shule za msingi Mtwara DC, Yegella ukosefu wa maji unazikumba shule hizo huku akiahidi kushirikiana na  mamlaka ya majia Mtwara ili kuweze kupeleke miradi ya maji.

Ametaja changamoto nyingi kuwa ni ukosefu wa walimu wa kutosha na amesema tayari ofisi yake imeshatuma maombi serikalini ili kuletea walimu kupitia ajira ya walimu 13,000 ambao serikali imetangaza kuajiri hivi karibuni

“Ni kweli tuna changamoto za walimu, lakini tunaishukuru serikaili imeshatangza nafasi za walimu 13,000 na sisi tumeshapeleka maombi ya kuomba kupewa walimu. Na wale walimu wanaotoka Mtwara waje watusaidie kufundisha watoto wetu,” amesema.







Choo cha zamani

No comments: