UJENZI WA BANDARI YA KISIJU UTATOA FURSA YA AJIRA KWA VIJANA NA KUINUA UCHUMI
IMEELEZWA kuwa ujenzi wa bandari ya kisiju utatoa fursa ya ajira kwa vijana na kuinua uchumi wanamkuranga na nchi kwa ujumla.
Akizungumza na wananchi wa vijiji tatu vya kata ya kisiju wakati wa kampeni Abdalah Ulega amesema lengo lake ni kuona bandari inafanya kazi ili vijana waondokane na umaskini na wapate uchumi.
Aidha ulega amesema bandari hiyo ya kisiju ambayo imekufa kutokana na mikoko kuota na mchanga kujaa ilikuwa inapokea mashua 12 kwa cku lakini sasa inapokea mashua moja,nisuala linalomuumiza lakini anapambana liweze kufanikiwa.
Ulega ameongeza kuwa ustawi wa kisiju ni bandari na barabara hivyo amewataka wananchi kuchagua chama cha mapinduzi ili kiweze kutatua changamoto zao.
Sanjari na hayo ulega amesema mpaka sasa zahanati tano zimefungulia, tisa zimekamilika ikiwemo zahanati ya koma na ishrini na sita zipo katika hatua mbalimbali.
Aidha ulega amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi kuondoa makundi baina yao na kuwa na umoja na mshikamano kuhakikisha wagombea wote wa chama cha mapinduzi kinashinda kwa kishindo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo(kusoto) akisisitiza jambo.
No comments: