NYAMBAYA AGAWA MIPIRA 250 KWA KANDA YA DAR ES SALAAM

Na Kaiza Pancras, Dsj

Mjumbe wa kamati ya utendaji TFF Lameck Nyambaya amekabidhi mipira 250 kwa wilaya tano za mkoa wa Dar es salaam kwa lengo la kukuza na kuendeleza mpira wa miguu.

Nyambaya amekabidhi mipira hiyo ambapo kila wilaya itapata mipira 50

Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Karume jijini Dar es salaam

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi mipira hiyo, Nyambaya amesema lengo la kutoa mipira hiyo ni kukuza na kuendeleza mpira wa miguu kwa mkoa wa Dar es salaam.

Katika mkutano uliohudhuriwa  na Rais wa TFF Wallace Karia,amempongeza mjumbe huyo kwa kukabidhi mipira hiyo kwa wilaya zote za jiji la Dar es salaam.

Karia amewaasa wadau wa mpira wa miguu kujitokeza katika maendeleo ya soka Tanzania.

"amefanya jambo kubwa sana kwa moyo wangu namshukuru sana, na wadau wengine mjitokeze katika kuinua mchezo wa mpira wa miguu kuanzia chini" amesema Karia

Alhaji Fahim Abdallah, Mwenyekiti wa kanda ya Kinondoni amesema " watatumia mipira hiyo katika kukuza soka la vijana wadogo "Grassroots" na kukuza la wanawake kanda ya kinondoni.

Mkutano huo pia  ulihudhuriwa na viongozi wa kanda zote za mkoa wa Dar es salaam na waandishi wa habari.
 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji TFF (Kulia) Lameck Nyambaya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi mipira kwa kanda ya Dar es Salaam, Kushoti ni Rais Wa TFF Walace Karia

No comments: