Njombe:Wanawake washindwa kutafuta uongozi kwa madai ya kukwamishwa na waume zao

Na Amiri Kilagalila, Njombe
BAADHI ya wanawake mkoani Njombe wamesema wameshindwa kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kutokana na kuzuiliwa na baadhi ya waume zao.

Wamesema nafasi ya mwanamke kwenye uongozi zimeendelea kupigiwa kelele kwaajili ya kutetea haki zao lakini wamekuwa wanahofia kuharibu ndoa na wengine wanazuiliwa na waume zao.

Nao baadhi ya wanaume mjini Njombe wamekili kutowaruhusu wake zao kuwania nafasi za uongozi kwa ngazi za ubunge na udiwani kwa kuhofia kuolewa na wanaume wengine na kusababisha ndoa kuvunjika.

Viongozi wa vyama vya siasa mkoani Njombe wamesema kuwa wametoa nafasi nyingi kwa wanawake kushiriki kuwania uongozi isipokuwa baadhi yao wamekuwa waoga kujitokeza.

Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Njombe Teresia Yomo amesema,kwa sasa wanawake wanaonesha ushiriki mkubwa kuwania nafasi za uongozi na kwamba mwanamke akiwa kiongozi atatetea haki za wanawake wenzao.

No comments: