NITAHAKIKISHA UCHUMI WA JIJI LA TANGA UNAAMKA UPYA NA KURUDI ENZI ZAKE-UMMY MWALIMU

 

Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Tanga Mjini atahakikisha Uchumi wa Jiji hilo unaamka upya kurudi enzi zake.

Ummy akizungumza katika mkutano wa Kampeni kata ya Nguvumali amesema kipaumbele chake kikubwa ni kufufua Uchumi wa Tanga kwakusukuma Ujenzi wa Viwanda vipya na kufufua vile vilivyokufa, Maboresho ya Bandari Awamu ya pili,Kusukuma Ujenzi  wa Bomba  la Mafuta kutoka Hoima-Chongoleani na kusimamia uwezeshaji Kiuchumi kwa akinamama na vijana.

Kukamilika kwa mipango hiyo kutazalisha ajira nyingi za mojakwamoja na kuongeza mzunguko wa fedha kwa wananchi na kufanya ustawi wao kiuchumi kuwa imara. 



 

 

No comments: