MBEYA CITY YAANZA MAZOEZI KUJINOA DHIDI YA YANGA SEPTEMBA 13

Na Agness Francis, Michuzi Tv
BAADA ya kula kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya KMC fc ikiwa ulikuwa ni mchezo wa kwanza ligi kuu Vodacom Tanzania bara ,kikosi cha Mbeya Fc leo asubui kimefanya mazoezi kujinoa kwa ajili mchezo wao unaofuata dhidi ya Yanga.

Yameelezwa hayo katika ukurasa wa Instagram wa timu hiyo ya Mbeya city iliyokita maskani yake Jijini Mbeya.

"Kikosi chetu kimefanya mazoezi Leo asubui kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea  mchezo wetu  unaofuata dhidi ya Yanga" ukurasa wa Instagram wa Mbeya City.

Mchezo huo wa pili utachezwa  septemba 13 katika  uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam majira ya saa moja jioni dhidi ya Wenyeji wao vijana wa Jangwani Yanga,

Ambapo timu ya Yanga  walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya wajela jela Tanzania Prison katika mchezo wa raundi ya  kwanza  uliopigwa katika  uwanja huo wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho cha Mbeya City kina kibarua kizito dhidi ya Yanga kutafuta alama tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri  kwa kupata matokeo mazuri ikiwa ni mwanzo wa ligi  ili kukwepa adhaa ya kucheza play of kama msimu uliopita 2019-20.  

Vijana hao wa Mbeya City  ambapo walinusurika kushuka daraja  ikiwa nafasi ya 15 na kujikusanyia alama 45 kibindoni na kulazimika kucheza play of dhidi ya Geita Sc iliopo dalaja la kwanza kwa kuanzia ugenini ambapo walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1

Katika mchezo wa marudiano Mbeya city waliwakaribisha Geita Sc katika dimba la uwanja wa Sokoine na Mbeya city kuibuka washindi kwa bao  1-0  kupitia kwa beki wa Geita kujifunga kwa kupiga kichwa cross ya mchezaji wa Mbeya City  Peter Mapunda,

Goli hilo lilidumu mapaka dakika 90 za mchezo kumalizika  na kuinusuru timu ya Mbeya city kusalia kubaki katika ligi kuu vodacomTanzania bara.

No comments: