" MAGUFULI AMEJENGA VITUO SITA VYA AFYA KONDOA TUMPENI KURA AMALIZE CHANGAMOTO YETU YA MAJI" -DITOPILE
Charles James, Michuzi TV
KATIKA kuendelea kutafuta kura za mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wabunge na Madiwani, Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ameshiriki uzinduzi wa kampeni Jimbo la Kondoa Mji na kuiombea kura CCM.
Ditopile amewaomba wananchi wa Kondoa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Makoa Ally pamoja na madiwani wote ili waweze kushughulika na shida ya maji inayowakabili wananchi wa Kondoa.
Amesema ndani ya miaka mitano ya Dk Magufuli Wilaya ya Kondoa imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo ikiwemo kujengewa miundombinu ya barabara, maboresho katika sekta ya Afya.
" Wote ni mashahidi hii barabara ya kutoka Kondoa kwenda Dodoma ilikua haipitiki, tungeweza kusafiri masaa hadi nane kutoka Kondoa hadi Dodoma mjini tena kwa gari, lakini leo ni masaa mawili tu umefika, yote haya ni kwa sababu ya Dk Magufuli.
Wilaya hiyo ilikua na shida kwenye eneo la afya, lakini Rais wetu alivyoingia miaka mitano tu tumejengewa vituo sita vya afya tena vya kisasa na vyenye ubora wa Hospitali za Wilaya, kwenye elimu nyinyi wote ni mashahidi sasa watoto wetu wanasoma bure kuanzia elimu ya Msingi hadi kidato cha nne," Amesema Ditopile.
Amewaomba wananchi wote kujitokeza Oktoba 28 kwenda kupiga kura za Ndio kwa CCM ili kumpa ushindi mkubwa Dk Magufuli aweze kumalizia kazi aliyokwisha kuianza ya kuwaletea maendeleo watanzania ikiwemo Kondoa.
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Kondoa Mji ambapo ameshiriki kumuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea Ubunge, Makoa Ally na Madiwani wa Kata zote za jimbo hilo.
Umati wa Wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Kondoa wakimsikiliza Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile alipokua akikiombea kura chama cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
Wazee wa kimila wa kabila la Warangi wilayani Kondoa wakimfanyia mila mgombea Ubunge wa Jimbo la Kondoa Mji, Makoa Ally kabla ya uzinduzi wa kampeni za Jimbo hilo.
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile akijadiliana jambo na mmoja wa wazee wa Wilaya ya Kondoa mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Kondoa Mji ambapo ameshiriki kuwaombea kura wagombea wa CCM akiwemo, Dk John Magufuli kwa nafasi ya Urais, Makoa Ally kwa nafasi ya Ubunge na Madiwani wa Kata zote.
Wananchi wakiwa na mabango mbalimbali yenye picha za mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kondoa Mji, Makoa Ally wakati wa uzinduzi wa kampeni za Jimbo hilo.
No comments: