MAGUFULI ACHAMBUA MADINI YA DHAHABU YANAVYOCHOCHEA KULETA MAENDELEO YA WATANZANIA


*Aaanika mipango, mikakati ya kuendelea kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo nchini

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Geita

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli ameelezea kwa kina mafanikio ambayo nchi yetu imeyapata kutokana na udhibiti na usimamizi thabiti wa fedha zinapatikana kupitia rasimali zilizopo nchini ikiwemo ya madini ya dhahabu ambayo yamekuwa yakinufaisha Watanzania wote.

Dk.Magufuli amesema hayo leo Septemba 9,2020 mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Geita wakati mkutano wake wa kampeni zake za kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia sekta hiyo ya madini na faida zake katika kuleta maendeleo nchini.

Wakati akizungumza na wananchi hao Dk.Magufuli alianza kwa kuelezea kufurahishwa kwake na mapokezi makubwa ambayo ameyapata tangu ameingia Geita na kwamba ana deni kubwa kwao."Mwaka 2015 nilikuja hapa kuwaomba kura , nanyi mkaniamini na kunichagua kuwa Rais wenu.Leo nimekuja tena kuomba kura ili nipate ridhaa.

"Ninaomba ridhaa kwenu kwasababu kama mnavyofahamu miaka mitano iliyopita tumefanya maendeleo mengi ikiwemo ya Mkoa wa Geita.Kwa Mkoa Geita umebarikiwa kwa kuwa rasilimali nyingi ambazo katika miaka mitano wamehakikisha zinanufaisha watanzania wote.

"Katika madini kumekuwepo na jitihada za kusimamia rasilimali ya madini, hivyo kwa Geita limeanzishwa soko kubwa la madini.Pia imetungwa sheria ya madini kwa ajili ya kusimamia vizuri rasiIimali hiyo pamoja na kuanzisha masoko, wachimbaji wadogo kuendelea na kushughuli za uchimbaji madini.

"Wananchi siku za nyuma ilikuwa wakigundua dhababu wanafukuzwa kisha wanakuja wengine lakini tukasema hapana, hivi sasa wananchi wakigundua madini wanapewa leseni wanaendelea kuchimba,"amesema Dk.Magufuli.

Akifafanua zaidi Dk.Magufuli amesema kutokana na udhibiti wa sekta ya madini ya dhahabu yameongezeka na kuongeza fedha ambayo inapatikana kwenye dhahabu"Mwaka 2016 dhahabu iliyouzwa ilikuwa kilo 337.482 ambayo thamani yake ilikuwa Sh.bilioni 22.5 na kutolewa mrabaha wa Sh.bilioni 1.2

"Baada ya kuchukua hatua dhahabu iliyouzwa na wachimbaji wadogo kwa mwaka jana(2019) ilikuwa kilo 4656.29 ambazo thamani yake ni Sh.blioni 375.5 na mrabaha wenye thamani ya bililioni 22.5.

"Wachimbaji wakubwa mwaka 2016 walichimba dhahabu kilo 17,587.15 yenye thamani dola za Marekani milioni 6.7.3 sawa na Sh.trilioni 1.4 na kutoa mrabaa dola za Marekani milioni 23.4 sawa na Sh. bilioni 53.81 lakini hadi Mei mwaka huu wachimbaji hao wameuza kilo 21,652.77 za dhahabu ambapo zimepatikana dola milioni 949.8 sawa na Sh.trilioni 2.2 na kutoa mrabaha wa Sh.bilioni 130.64.

"Bila kubana na kuweka mikakati fedha hizo ambazo zinapatikan sas zisingeonakana, tangu Dunia iuumbwe yamepotea matrilioni mangapi? Tangu enzi za ukoloni zimepotea fedha kiasi gani kutokana na dhahabu tunaliyonayo.Ikiwa mwaka mmoja tumetengeneza Sh.trilioni 2.2.

"Tujiulize maswali nchi hii imepoteza trilioni ngapi?Haya ndio maswali ya Watanzania kuanza kujiuliza na ndio maswali ya msingi, ndio maswali ya msingi ambayo wagombea wenzangu wanatakiwa kujiuliza na kueleza nini watafanya,"amesema Dk.Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza ukindoa mamilioni ya watu wanaofuatilia kupitia vyombo vya habari mbalimbali nchini.

Hata hivyo Dk.Magufuli amesema Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020 pamoja na mipango ya Serikali iliyopo ni kwamba wamepanga kuongeza maeneo ya wachimbaji wadogowadogo na wataendelea kuwapatia leseni , mafunzo, mitaji na teknolojia rahisi."Na haya yote yamewekwa yamewekwa kwenye Ilani ya CCM ya uchaguzi wa mwaka huu. Tunaomba mtuchague ili haya ambayo tumeyapanga yasije kupotelea hewani.

Pamoja na mambo mengine amesema kuwa fedha ambazo zinapatikana kutokana na dhahabu imekuwa sehemu ya fedha zinazokwenda kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini kupitia miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa.

No comments: