MAFUNZO MAALUMU YA USIMAMIZI WA FEDHA KUTOLEWA IFM




Na mwandishi wetu, Michuzi TV

 CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeandaa mafunzo maalumu ya usimamizi wa madeni na rejesho  yenye mlengo wa kuwawezesha washiriki kuelewa zaidi kuhusiana na usimamizi huo kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chuo hicho, imeelezwa kuwa mafunzo hayo yatafanyika katika chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Septemba hadi Septemba 30 mwaka huu.

Aidha imeelezwa kuwa mafunzo hayo yamewalenga mameneja mikopo na Fedha, maafisa uhusiano na wakaguzi.

Imeelezwa kuwa mafunzo hayo  yatabeba mada mbalimbali ikiwa pamoja na; Usimamizi wa madeni na marejesho, sera za usimamizi wa mikopo,ufuatiliaji na tathimini za mikopo pamoja  na mikakati na mbinu za ukusanyaji madeni.

Vilevile imeelezwa kuwa ada ya ushiriki wa mafunzo hayo ni shilingi 900,000/=   itakayohusisha ada, nyaraka na chakula.

Washiriki wa mafunzo hayo wameelekezwa  kuwasiliana na Dkt. E.Mwambuli kupitia barua pepe Erick.mwambuli@ifm.ac.tz au  0713 537913/0754 338767 mara baada ya kufanya malipo hayo.

No comments: