KONGAMANO LA PSPTB KUKUTANISHA WADAU ZAIDI YA 1000, KUJADILI CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA UNUNUZI NA UGAVI
Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeandaa kongamano litakalowakutanisha wataalam hao lengo ni kujadili jinsi gani ya kufikia ubora ili kuongeza thamani katika Sekta ya ununuzi na ugavi kutokana na chamgamoto mbalimbali za Ununuzi na Ugavi katika Sekta za Umma na Binafsi.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Matendaji wa bodi hiyo, Godfred Mbanyi amesema kongamano hilo litawakutanisha wadau zaidi ya 1000 kutoka Ndani na nje ya Nchi ili kupeana uzoefu kutokana na sekta hiyo kuwa nyeti katika kuongeza pato la Taifa ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali.
Mbanyi amesema katika Kongamano hilo Wataalamu hao watapata nafasi ya kujadili, kuchambua, kuweka mikakati ya uboreshaji katika Sekta ya Ununuzi na Ugavi katika Ununuzi wa Umma na Kampuni Binafsi.
"Michakato ya Ununuzi na Ugavi katika Sekta ya Umma maana take tunatoa huduma nzuri kwa Wananchi, pia mchakato huo unapoenda vizuri basi Serikali inapata Kodi", amesema Mbanyi.
Amesema Sekta ya ununuzi na ugavi inaposimamiwa vizuri inasaidia Serikali kupata mapato yake hivyo kongamano hilo litasaidia wadau hao kutoa fursa kwa wafanyabiashara pamoja na Makampuni kutangaza Biashara zao.
Kongamano hilo ni la 11 ambalo linatarajiwa kufanyika Jijini Arusha Disemba 2 hadi 5mwaka huu, huku miongoni mwa Nchi zinazotarajiwa kushiriki ni pamoja na Nchi ya Kenya, Rwanda, Burundi pamoja na Uganda.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uandaaji wa kongamano litakalowakutanisha Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lengo ikiwa ni kujadili jinsi gani ya kufikia ubora ili kuongeza thamani katika Sekta hiyo. Kongamano hilo ni la 11 linatarajiwa kufanyika Jijini Arusha Disemba 2 hadi 5 mwaka 2020.
Baadhi ya wajumbe wa kongamano litakalowakutanisha Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Kongamono hilo litakalofanyika mkoani Arusha.
Baadhi ya wajumbe wa kongamano litakalowakutanisha Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Kongamono hilo litakalofanyika mkoani Arusha.
Kaimu Mkurugenzi Matendaji wa bodi hiyo, Godfred Mbanyi (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa watakaosimamia maandalizi ya Kongamano hilo mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za PSPTB jijini Dar es Salaam
No comments: