KITUO CHA KUPOZA UMEME ZUZU KUZALISHA MEGAWATI 250

 



Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt.Alexander Kyaruzi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho  kilichopo jijini Dodoma.

Mratibu wa Mradi wa kituo cha kupoza umeme Zuzu, Mhandisi Peter Kigadye,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt.Alexander Kyaruzi  akiongoza wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO  kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho  kilichopo jijini Dodoma.MWENYEKITI Wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),  Mhandisi Alexender Kyaruzi  amesema kuwa upatikanaji wa umeme utaimarika baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu jijini hapo ambacho kitazalisha umeme wa Megawati 250.

Mitambo unaofanya kazi katika  kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.
Na Ripota wetu, Michuzi TV

 MWENYEKITI Wa bodi  ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),  Mhandisi Alexender Kyaruzi  amesema kuwa upatikanaji wa umeme utaimarika baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzukilichopo  jijini Dodoma ambacho kitazalisha umeme wa Megawati 250. 

Kauli hiyo ameitoa leo  jijini Dodoma  wakati wa ziara yake ya kutembelea na  kukagua ujenzi huo iliyofanywa na bodi hiyo.

Aidha Mhandisi Kyaruzi ameeleza kuwa  kwasasa kituo kinazalisha Megawati 48 ambazo haziwezi kutosheleza kutokana na ongezeko la watu kwa mkoa huo.

“Baada ya kukamilika kwa kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 250 ambapo ukizijumlisha na Megawati 48, kitakuwa na takribani Megawati 300 ambao utakuwa umeme mwingi sana”ameeleza Mhandisi Kyaruzi.

 Mhandisi Kyaruzi amesema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Septemba 15 mwaka huu na Septemba 30 wataanza kufanya majaribio ya uzalishaji wa umeme hali itakayoongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa mkoa wa Dodoma.

“Kituo hiki kikikamilika tunaamini kabisa tutakuwa na Umeme mwingi na wa uhakika mana kwa sasa zinazalishwa Megawati 48, lakini kikikamilika kitazalisha Megawati 250, huu ni Umeme mwingi sana,”amesisitiza.

Kwa upande wake  Mratibu wa mradi wa kituo hicho, Mhandisi Peter Kigadye, ameeleza kuwa  kituo hicho kitakuwa kikipokea umeme kilovati 400 na kupooza kwenda 220 hadi 33.

Pia Kigadye ameweka wazi kuwa mwakani wanatarajia kujenga laini 8 imara na za uhakika ambazo zitawezesha kutawanywa umeme katika mkoa mzima wa Dodoma na viunga vyake.

“ Baada ya kukamilika kwa kituo hiki tunatarajia kujenga vituo vya umeme(substation), Wilaya ya Kongwa na mji wa serikali vyote vitakuwa na uwezo wa kuongeza usambazaji wa umeme wa uhakika”, amesema Kigadye.

No comments: