DKT. TULIA ATANGAZA SAA YA NEEMA MBEYA

 




Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM Dr. Tulia Ackson ameshiriki kampeni za kunadi sera za chama chake katika kata ya Iganzo jijini humo ambapo amewataka Wananchi kupiga kura zote za kishindo na Chama Cha Mapinduzi itapofika siku ya October 28, 2020 ili wayapate maendeleo ya kweli kupitia Serikali ya awamu ya tano. 

Dr. Tulia ambaye alikuwa ameambatana na baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya pamoja na mchekeshaji Emmanuel Mathias maarufu kama MC PILIPILI amesema>>> 

“Ndugu zangu kama ambavyo nasisitiza siku zote kwamba CCM tuna hoja na wenzetu wana vihoja, chagueni viongozi wanaotatua changamoto zenu na sio wanaotoa malalamiko kila kukicha. Hapa Mbeya tunataka Mbunge wa kujiongeza hivyo basi safari hii tusifanye makossa katika kuchagua” -Dr. Tulia Ackson 

“Kwenye eneo la afya mimi nilishakuja hapa kwenye zhanati Iganzo na nikaleta kitanda cha kujifungulia wakinamama na mashuka, sisi tunataka ukija hapa Iganzo usitupe stori tu bali tueleze umefanya nini. Kama hatukuwahi kukuona kwenye shule zetu, hatukukuona kwenye zahanati basi safari hii Mbeya mjini tutachagua mtu tuliyekata naye kuni ndio tutakayeota naye moto”-Dr. Tulia Ackson 

“Sisi ni watu wa kazi na watu wa kujiongeza, tunaposema hivyo tunamaanisha kweli kweli. Na leo ni vile muda hautoshi tungewaleta hapa baadhi ya wazee hapa Mbeya jiji ambao kwa kupitia kwangu kama mbunge wa Connection tumewasaidia bima za afya bure kwa kupitia Tulia Trust, acha hilo tu kwenye uwezeshaji kiuchumi tumewawezesha mikopo ya riba nafuu Wakinamama, Vijana na hata wazee. Sasa huo ni mwanzo tu chagueni Tulia awe Mbunge wenu mjionee makubwa mengine”-Dr. Tulia Ackson

No comments: