AMANI YETU, UTULIVU NA MSHIKAMANO NI KWA SABABU YA DINI-MAJALIWA

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akiongea na wananchi waliouthuria katika Tamasha la maombi lililoandaliwa na radio safina juzi lililofanyika katika viwanja vya magereza mkoani Arusha ambapo aliwasihi wananchi kuendelea kudumisha amani yetu.
(Picha na Woinde Shizza , ARUSHA).

Na Woinde Shizza, Michuzi Tv Arusha
AMANI, Utulivu na mshikamano ni matokea chanya ya kuwa na nchi yenye dini zilizo imara katika kuombea hivi vitu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, alipokuwa akizungumza na waumini wa kanisa la Safina jijini Arusha.

Alisema kutokana na maombezi ya waumini wa dini zote ndio maana nchi ya Tanzania imeweza kushinda vita mbalimbali vikiwemo vya uvamizi wa wadudu aina ya Nzige na ugonjwa wa Corona.

Aliwataka watanzania wote kuendelea kuiombe nchi yetu na pia kuombea viongozi watakaorudi kwenye madaraka wakawe viongozi wenye hofu ya Mungu na wapenda kutenda haki.

Aidha, aliwahimiza waumini wote kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kuchagua viongozi watakaependa maendeleo ya nchi na kuwa viongozi bora

Akitoa salamu za Mkoa wa Arusha kwa niaba ya wananchi wote, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta, alisema wana Arusha wanaishi kwa kumtegemea Mungu kwa kila kitu.

Pia, aliwahasa wananchi wa Arusha kuto kukubali kugombanishwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Aliwataka wana Arusha wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi na kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo.

Waziri Mkuu amehitimisha ziara yake ya kampeni za uchaguzi Mkoani Arusha kwa kufanyiwa maombi maalumu katika tamasha la maombi lililoandaliwa na kanisa la Safina Jijini Arusha.

No comments: