Waziri Hasunga atoa siku 5 Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kukamilisha malipo ya wakulima wa Korosho Kibiti na Mkuranga



Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga(Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa Korosho, Maafisa Ugani, na wadau mbalimbali wa Kilimo katika Wilaya ya Mkuranga akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Pwani. (Picha Zote Na Innocent Natai)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga(Mb) akizungumza na moja ya
Wakulima wa Korosho Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani, Jana Tarehe 13 Agosti 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga(Mb) akisalimiana na viongozi
wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Kibiti Mkoani Pwani. Jana Tarehe 13 Agosti 2020.

Na Innocent Natai, Pwani

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa sikuTano kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania(CPB), Viongozi wa Vyamavya Ushirika pamoja na Benki ya Kilimo, kuhakikisha wanakutana na wakulima waKorosho Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani ambao fedha zao za mauzo ya Koroshohazijalipwa mpaka sasa ili kuwalipa haraka iwezekanavyo.

Amewataka kukagua taarifa zao na kuwalipafedha zao mara moja kwani serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania DktJohn Pombe Magufuli ilishatoa fedha zote kwa ajili ya kufanyika kwa malipo hayo, "Nasikitika kwanini mpaka sasa malipo hayajakamilika" Aliuliza Waziri Hasunga

Akizungumza mbele ya Wakulima na Maafisa ugani Waziri Hasunga amesema kuwa inasikitisha kuona bado kuna wakulima wanaidai serikali
angali serikali kupitia kwa Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imekwisha kutoafedha kwa ajili ya kuwalipa kwa muda mrefu kitendo kinachowafanya wakulimakuichukia serikali na kukata taama ya kufanya kilimo.

Amesema kuwa kumekuwa na kisingizio cha muda mrefu kuwa baadhi ya wakulima taarifazao za kibenki zina makosa hivyo kusababisha kushindwa kufanyiwa malipo kwanjia ya kibenki jambo hili siwezi kukubaliana nalo.

“Nilitoa siku 14 kuhakikisha kuwa wakulima wa
Korosho Wilaya ya Mkuranga wawe wamemaliza kulipwa fedha zao lakini mpaka sasabado natoa siku tano Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
Tanzania(CPB), viongozi wa Vyama vya Ushirika pamoja na Benki ya Kilimo
kuhakikisha hili suala linamalizika” Alisema Hasunga

Aidha, Hasunga ametoa siku mbilikwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania CPB kuhakikishawanabandika majina ya Wakulima waliolipwa fedha zao za Korosho kuanzia Mwezi
Januari 2020 kwenye mbao za matangazo ili kuwasaidia wakulima kutambuawalikwisha kulipwa fedha zao na ambao bado ili pia serikali kuweza kubainiudanganyifu unaofanywa katika malipo.

Pia amesema serikali kupitia Wizara ya Kilimona Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga imewakamata na itaendelea kuwakamataviongozi wa vyama vya ushirika wanaofanya ubadhilifu wa mali za wanaushirika,
pia na waliofanya ubadhilifu na wizi kwenye uuzaji wa Korosho msimu uliopita

Hivyo, Hasunga amewataka wakulima kuendeleakuvumilia wakati serikali ikiendelea kuwafuatilia na kuwakamatawaliofanya wizi wa kuuza korosho za wakulima bila kufuata utaratibi na kuwalipaWakulima hao.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga mbali nakutembelea, kusikiliza na kutatua kero za Wakulima wa Korosho Wilayani MkurangaMkoani Pwani alifika pia kuzungumza na wakulima Wilayani Kibiti Mkoani hapohuku akiendelea kutoa maagizo ya kuhakikisha wakulima wa Korosho wanalipwastahiki zao kwa wakati na waliofanya udanganyifu na kuuza korosho za wakulimakuchukuliwa hatua za Kisheria.

No comments: