WATU WASIOJULIKANA WATEKETEZA NYARAKA ZA CHADEMA
Muonekano wa wa ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mbeya Mjini.
Nyaraka zikiwa zimeungua Moto ndani ya Ofisi za CHADEMA Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ikiwa imeweka utepe kutokuruhusu mtu kuingia katika ofisi za CHADEMA zilizopo Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya.
JESHI la Polis Mkoa wa Mbeya Mtu au watu wasiofahamika walichoma moto nyaraka mbalimbali zilizokuwa ndani ya ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mbeya Mjini.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulricho Mtei imeeleza kuwa nyaraka hizo zilichomwa Mnamo tarehe 19.08.2020 majira ya saa 09:00 usiku huko Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Ofisi hiyo ni ya chumba kimoja ambacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo wamepanga kwenye nyumba ya Anna Abel Mwansasu.
"Mbinu iliyotumika ni kuvunja kufuri la mlango wa ofisi, kuingia ndani kisha kutoa baadhi ya nyaraka zilizokuwa kabatini, kuziweka sakafuni kisha kuzichoma moto.
Nyaraka hizo ni pamoja na fomu za matokeo ya kura za maoni kwa wagombea nafasi ya Udiwani, viti maalum wanawake jimbo la Mbeya mjini ambazo zilitakiwa kusafirishwa leo tarehe 19.08.2020 kwenda Makao Makuu ya CHADEMA Dar es Salaam ili zipelekwe Tume ya Taifa ya Uchaguzi." Imeeleza taarifa hiyo
Aidha vitu vingine vilivyochomwa moto ni pamoja na viti vinne [4] vya plastiki na mlango mmoja [1] wa kabati lililokuwa limehifadhi nyaraka hizo kwani Odisi hiyo haina Mlango.
Thamani ya mali iliyoteketea bado kufahamika, Kiini cha tukio kinachunguzwa japo uchunguzi wa awali umebaini kuwa kulikuwa na hali ya kutoridhika kwa baadhi ya wajumbe au wagombea kuhusiana na matokeo ya kura za maoni za Viti Maalum na Udiwani.
Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia ikiwa ni pamoja na msako wa kuwakamata wahusika kwa hatua zaidi za kisheria.
No comments: