VIJANA WATAKIWA KUONDOA DHANA YA KUAJIRIWA

 mkuu wa chuo cha Uhasibu, Profesa Eliamani Sedoyeka.

Na Woinde Shizza, Michuzi Tv Arusha
VIJANA wametakiwa kuondoa dhana ya kutegemea kuajiriwa badala yake wajijengee dhana ya kujiajiri wenyewe ili waweze kuendelea na kujiendeleza kwa mandeleo ya taifa lao kwa ujumla

Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo cha Uhasibu, Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa ni vyema vijana kuanza kujiongeza na kujijengea dhana ya kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao na kuacha kutegemea kuajiriwa

Alisema wao kama chuo cha uhasibu mkoa wa Arusha wameanza kubadilishwa mitaala ambapo mbali na kufundisha masomo ya fedha na IT pia wameanza kufundisha vijana mbinu mbalimbali za ujasiriamali ambapo wanampa mwanafunzi kutoa malengo yake katika eneo lolote lile wanaweza wakavutiwa ili waweze wakajiajiri wakimaliza masomo yao.

“ Sisi kama chuo kunawanafunzi wameanza kujitokeza na kuleta mawazo yao ya biashara na sisi wanapokuja tunawashika mikono na tunawasaidia kuboresha wazo lao pia niseme tumeshaanza kupata wadau mbalimbali ambao wanaweza kutuzamini kitu tunachofanya ni kusikiliza wazo la mwanafunzi na kuliboresha zaidi baada ya hapo tunamfunisha mwanafunzi na kupatia mdau ambae atampa mkopo kwa ajili ya kuanza kutendea kazi wazo lake “alisema Sedoyeka

Aidha alibainisha kuwa wao kama chuo wanajeshi kubwa la vijana ambapo wamejipanga vyema na kuweka mikakati ya kuwaelimisha vijana kutumia kilimo kama fursa ambapo alisema wamekuwa wakiwaambia vijana japo wanasoma maswala ya fedha pamoja na IT lakini kwa sasa ni vyema pia vijana kuangalia kilimo kama ni fursa .

“Na uzuri kilimo kinasaidia na kinaweza kufanyika sehemu yeyote kama vile nyuma ya nyumba au kijana pia anaweza ata kukodisha shamba kwa ajili ya kilimo na kuwaamasisha kuwa kilimo sio kitu kigumu hivyo anaweza kujiajiri au kuajiri vijana na nisema katika maonyesho haya ya nane nane tumeweza kutoa elimu ka vijana na wajasiriamali mbalimbali na hatutaishia hapo tutatendelea kutoa elimu zaidi ili hawa vijana waweze kujiajiri na kuajiri wengine”alibainisha Sedoyeka

Aidha pia alisema katika maonyesho ya nane nane wameweza kuwafundisha wajasiriamali mbalimbali elimu ya namna ya kuboresha mawazo ya kibiashara, tumewajengea uwezo wa kimasoko pamoja na uwezo wa namna ya kutunza fedha zao.

Chuo hichi cha Uhasibu Arusha katika maonyesho haya ya nane nane kimeweza kushika nafasi ya pili kwa kanda katika eneo lautoaji wa elimu katika maonyesho haya.

No comments: