TAMWA YAANGUKIA NEC,YAOMBA KUWEKWA SHERIA KALI

Mkurugenzi CHAMA cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA), Rose Rubean.

CHAMA cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuweka sheria kali kwa makundi na viongozi ambao nafasi zao kuwadhalilisha na kubana nafasi ya wanawake kushiriki katika uchaguzi mkuu.

CHAMA cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuweka sheria kali kwa makundi na viongozi ambao wanatumia nafasi zao kuwadhalilisha na kubana nafasi ya wanawake kushiriki katika uchaguzi mkuu.

Hao yamesemwa na Mkurugenzi wa TAMWA, Rose Rubean jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa takwimu zinaonyesha ni wanawake wawili tu ambao wamejitokeza kugombea nafasi ya juu ya urais pia wanawake watano wakitambulishwa kuwania nafasi ya umakamu wa urais, hii ikionyesha ushiriki mdogo sana wa wanawake kujitokeza hali inayopelekea kuziweka bayana changamoto zinawakabili wanawake.

Aidha, imeelezwa kuwa lugha za kudhalilisha kwa wanawake hasa katika kipindi cha uchaguzi huwadhoofisha sana wanawake huku wakizitaka mamlaka husika kudhibiti vitendo vya rushwa ya pesa na ngono kwa kuwa huleta adha kubwa kwa jamii.

Rose ameziomba pia jumuiya mbalimbali za wanawake kwenye vyama vya siasa kuhakikisha uwazi unakuwepo pamoja na uthubutu wa wanawake kuzidi kujitokeza zaidi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

No comments: