St. Anne Marie yapeleka kidato cha sita wote vyuo vikuu
Wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri wakishangilia na Makamu Mkuu wa shule hiyo, Ambroce Mrosso, baada ya wanafunzi wote wa kidato cha sita wa shule hiyo kufaulu kwa daraja la 1, II na III na kupata sifa za kujiunga na
vyuo vikuu mbalimbali kwenye mitihani hiyo.
Makamu Mkuu wa shule ya St Anne Marie Academy iliyoko Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, Ambroce Morosso, akiwanaisi wanafunzi wa kidato cha tano kusoma kwa bidii ili kupata matokeo mazuri kama wenzao wa kidato cha sita ambao wote wamefaulu na kupata sifa za kujiunga na vyuo vikuu kwa kupata daraja la I, II na wachache daraja la III.
Na Mwandishi Wetu
SHULE ya St Anne Marie Academy ya jijini Dar es Salaam imefanikuwa kufaulisha wanafunzi wake wote kujiungana vyuo vikuu katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa juzi.
Matokeo hayo yalitagazwa mwishoni mwa wiki na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ambapo wanafunzi 18 wa shule hiyo wamefanikuwa kufaulu kwa daraja la kwanza.
Mkuu wa shule hiyo iliyoko Mbezi kwa Msuguri , Gladius Ndyetabura alisema kwenye matokeo hayo wanafunzi 68 wa shule hiyo wamefanikiwa kupata daraja la pili na 88 daraja la tatu.
Alitaja siri ya mafanikio ya shule yake kuwa ni usimamizi mzuri na ufuatiliaji wa taaluma na kwamba shule imekuwa ikiwapa motisha wanafunzi wa shule hizo na ndiyo sababu imekuwa ikipata matokeo mazuri kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa.
"Shule ikiwa na mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia kama vile vifaa vya kutosha, madawati, maji, maktaba ya kisasa, walimu wenye ari na wanafunzi kula chakula kizuri na cha kutosha lazima utapata matokeomazuri,” alisema Ndyetabura
Alisema wanatarajia kuanza kuwapeleka nchini Dubai, Uingereza hadi Marekani wanafunzi watakaokuwa wanafanya vizuri kwenye mitihani yao ili iwe chachu kwa wengine kufanya vyema kwenye mitihani ya ndani na ile ya kitaifa.
"Shule imejiwekea utaratibu wa kuwapa motisha wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi na huwa tunakawaida ya kuwapeleka mbuga za wanyama kama Serengeti, Mikumi, Ngorongoro hivyo tutaanza kuwapeleka Ulaya," alisema
Alisema mwaka jana wanafunzi wa msingi na sekondari wa shule hiyo waliofanya vizuri walipelekwa kutembelea Bunge ambako walijifunza mambo mbalimbali na kwamba utaratibu huo utakuwa endelevu.
Aliwashukuru wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo akisema kuwa matokeo hayo mazuri ni matokeo ya uwekezaji uliofanywa na wazazi hivyo aliwahimiza wasichoke kuwekeza kwani manufaa yake watayaona baadaye.
No comments: