SPIKA JOB NDUGAI ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE WA JIMBO LA KONGWA
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akabidhiwa fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kongwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Dkt. Omary Nkullo tukio lililofanyika leo katika Ofisi za Halmashuri hiyo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongozana na Wachama mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Jimbo la Kongwa wakati akienda kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la hilo tukio lililofanyika leo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akionyesha fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kongwa aliyokabidhiwa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Dkt. Omary Nkullo (hayupo kwenye picha) tukio lililofanyika leo katika Ofisi za Halmashauri hiyo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Dkt. Omary Nkullo wakati akielezewa utaratibu kabla ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kongwa tukio lililofanyika leo katika Ofisi za Halmashauri ya Kongwa Mkoani Dodoma.
No comments: