SERIKALI YARIDHISHWA NA HATUA ZINAZOENDELEA KATIKA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA PAPU
Katibu Mkuu mtendaji wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Dkt Zainabu Chaula akizungumza na Waandishi was habari Mara baada ya kukagua ujenzi wa Maendeleo ya ujenzi wa makao ya Posta Afrika,kushoto kwake Ni Katibu Mkuu mtendaji Picha zote na Vero Ignatus.
Katibu Mkuu mtendaji wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Zainabu Chaula akipewa maelezo namna ujenzi wa jengo la Makao makuu ya Posta Afrika unavyoendelea
Katibu Mkuu mtendaji wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Zainabu Chaula akitokw katika Ofisi za PAPU kuelekea kukagua ujenzi unavyoendelea
Na.Vero Ignatus,Arusha
Siku chache Mara baada ya kuanza kwa Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Africa linalojengwa Jijini Arusha, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano imeridhishwa na hatua zinazoendelea katika Ujenzi wa Jengo hilo huku ikikiri kuwa kuwepo kwa Makao Makuu hayo ya Posta Duniani hapa nchini Yataongeza ukuaji wa Biashara ya Posta nchini.
Dkt.Zainab Chaula ni Katibu Mkuu wa ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano amesema kuwa Mradi huo ni mkubwa wa kimkakati,unaohusisha mahusiano ya Kimataifa ,ambao ni Umoja wa watoa huduma wa posta duniani ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa Msimamizi.
Amesema nchi ya Tanzania ina manufaa makubwa na Mradi huo kwani ndiyo wanatoa Ardhi,Mradi huo unatakiwa ufanyike ndani ya miaka 3 hivyo utakamilika june 2022 ambapo ulianza rasmi Januari 2020 ukizinduliwa rasmi na Mhe Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isac Kamwelwe,hiyo yeye kama mtendaji anao wajibu wa kuhakikisha mipango hiyo inakamiliia kwa wakati ukiokusudiwa.
Amesema kutoka June -augusti 2020 yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana kwasababu kazi inaendelea na wanafuata kanuni na taratibu zote ambapo Watanzania zaidi ya 70 wamepata Ajira
Alimshukuru Rais kwa kutoa sehemu ya fedha kwaajili ya Mradi huo, na kukiri kwamba Posta haijafa ipo kiganjani kupitia sekta ya mawasiliano na kusema huduma zimekuwa kwa asilimia kubwa, hivyo wataendelea kuimarisha kwa kupitia Umoja huo ambao una nchi zaidi ya 52 Afrika amesema kitendo cha kuwepo mradi huo nchini watafanya vizuri zaidi kwasababu ni fursa ya kibiashara ambapo biashara ya posta inatazamiwa kukua Mara 100 zaidi kuliko ilivyo Sasa.
Katibu Mkuu wizara ya Ardhi nyumba Maendeleo ya makazi Bi. Mary Makondo ameishukuru serikali kuwezesha Mradi huo wa mkakati na kusema kuwa kama nchi tutapata manufaa makubwa ya kuwepo kwa mtekelezaji wa Mradi huo kwaajili ya PAPU
Amesema Tanzania umenufaika kwa kupata ardhi iliyowezesha Mradi kutekelezeka,ajira na wanatarajia wananchi haswa wakazi wa Arusha wataendelea kupata ajira zaidi kulingana na nahitaji na utekelezaji wa Mradi.
Kwa upande wake Injinia Hanton Kajiraki msimamizi Mkuu wa Mradi anayefanya kazi kwa niaba ya serikali kupitia TCRA na PAPU amesema Mradi huo unatofauti kubwa kutoka June hadi octoba kwani wameshachimbia hadi Sasa pails 145 ambapo ni zaidi ya 75% hivyo wanategeme kumaliza zoezi la kuchimbia pails mwishoni wa August
Amesema mradi huo utagharimu jumla ya shilingi billioni 33.7 ambapo ni jengo la ghrorofa 17 hadi sasa changamoto siyo kubwa sana kwani kazi unaenda kama walivyokwisha kupanga .bil 33.7 ni jengo la gorofa 17
Mwisho
No comments: