RC Njombe awapa siku saba TBA kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo ya ofisi za mkoa

Na Amiri Kilagalila, Njombe
MKUU wa mkoa wa Njombe Mhandisi Mwita Marwa Rubirya, amewaagiza wakala wa majengo Tanzania TBA mkoa wa Njombe kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi jengo la ofisi ya mkoa wa Njombe ndani ya siku kabla serikali kulazimika kusitisha mkataba wao na kuandaa utaratibu mwingine wa ukamilishaji wa kazi hiyo ulionza Oktoba, 2017.

Mkuu wa mkoa wa Njombe ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo linalojengwa Lunyanywi mjini Njombe na kubaini udhaifu kwenye utekelezaji.

“Mkandarasi ni TBA ambaye alitakiwa awe amekamilisha kazi hii June mwaka huu baada ya kukagua tumeona udhaifu mkubwa kwenye upande wa utekelezaji,na vifaa ni vichache kama mnavyoona lakini hata watendaji hawaridhishi”alisema Rubirya

Aidha Rubirya ameongeza kuwa
“Kwa hiyo tumetoa maelekezo kuwa TBA wahakikishe wanaleta vifaa na wataalamu ili kuhakikisha kazi hii inakwenda kwa kasi ili tuweze kukamilisha mradi huu na tumewapa angalizo wasipofanya kazi hiyo ndani ya siku saba kubadilisha hali ya utendaji,tutalazimika kusitisha mkataba wao ili kuandaa utaratibu mwingine wa kukamilisha kazi hii.

Kaimu meneja wakala wa majengo TBA mkoa wa Njombe Mhandisi Herman Daudi Tanguye,amesema mradi wa ujenzi wa ofisi hizo unaoghalimu zaidi ya bilioni 5.6 unakabiliwa na changamoto nyingi hivyo anaamini utakamilika Februal 17,2021 endapo taratibu za kifedha zitaendelea vizuri.

“Mradi una changamoto nyingi,jambo la kwanza ni upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kwa mfano mchanga unapatikana zaidi ya KM 60 kutoka eneo la mradi na Njombe kuna mvua nyingi na jengo hili limejengwa eneo ambalo halina barabara lakini tumewasiliana TARULA mara kadhaa ili angalau waweze kutungenezea barabara”alisema Tanguye

Vile vile amesema Changamoto nyingine ni kutokana ugumu wa upatikanaji wa kokoto zinazopatikana maeneo machache ikiwemo Chalinze mkoani Pwani pamoja na uguu wa upatikanaji wa Mafundi na vibarua ambao mara kwa wamekuwa wakipatikana wilaya za jirani ambao wamekuwa wakishindwa kufanya kazi kulingana na mazingira.

Aidha amesema wamepkea maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Njombe na kuhakikisha ndani ya kipindi hicho yanatekelezwa.
 Kaimu meneja wakala wa majengo TBA mkoa wa Njombe Mhandisi Herman Daudi Tanguye akifafanua sababu zilizopelekea kuchelewa kukamilika kwa mradi huo ulioanza mwaka 2017.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Mwita Marwa Rubirya wakati akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo wa ujenzi unaoendelea mjini Njombe.

No comments: