RAIS DKT.SHEIN AJUMUIKA NA VIONGOZI,WANANCHI MAZIKO YA JUMA RESI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi AlhajjDk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Juma Khais Haji (Juma Resi) maziko yaliofanyika Kijijini kwao Upenja Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua baada ya kuhitimishwa kwa hitma ya Marehemu Juma Khamis Haji (Juma Resi) aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani Kichama, iliofanyika katika msikiti wa Kiwengwa na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.Sheikh. Hassan Othman Ngwali na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi. (Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj
Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Juma Khamis Haji (Juma Resi) alipofika nyumbani kwa marehemu Kijiji cha Upenja na (Kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hasssan Othman Ngwali.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Balozi Seif Ali Iddi , wakijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua baada ya kumaliza Sala ya kuusalia Mwili wa Marehemu Juma Resi, iliofanyika katika Msikiti wa Upenja Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi AlhajjDk. Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wa Serikali na Wananchi katika maziko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani Kichama Juma Khamis Haji (Juma Resi) yaliofanyika Kijiji kwao Upenja Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.22/8/2020.(Picha na Ikulu)VIJANA wa Chipukizi wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Juma Khamis Haji (Juma Resi) wakielekea katika eneo lililloandaliwa kwa ajili ya maziko kijijini kwao Upenja Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)

No comments: