PROFESA PARAMAGAMBA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akimpokea Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi kwenye Banda la SUA kabla ya kuzindua rasmi maonesho hayo ya Wakulima nanenane Kanda ya Mashariki.
 Prof. Paramagamba Kabudi akipokelewa.
 Prof. Paramagamba Kabudi akipokea maelekezo
 Mazungumzo yakifanyika.
  Mazungumzo yakifanyika.






Na Calvin Gwabara


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi apongeza kazi kubwa inayofanywa na Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA katika kuboresha Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kuleta tija kwa Taifa.

Mhe. Prof. Kabudi ameyasema hayo alipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Kanda ya Mashariki kabla ya kwenda jukwaani kuzungumza na Wananchi,waoneshaji na wadau wengine wa Kilimo wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.

“ Chuo Kikuu hiki cha SUA mnafanya kazi nyingi na nzuri kwa faida ya nchi hii lakini niw aombe Muongeze jitihada za juzi tangaza kazi hizi ili watu wengi zaidi wazijue na kunufaika nazo maana zinahitajika sana na Wakulima, wafugaji na Wavuvi” Alisisitiza Mhe. Prof. Kabudi.

Amesema kuna kila sababu ya SUA kuona sasa umuhimu wa kuanzisha Mashamba ya Miti Dawa badala ya kutegemea kuvuna porini sasa ziwepo jitihada za makusudi za kuhamasisha watu kupanda akitolea mfano nchi kama madagaska ambao wameanza kutoa miti Dawa porini  badala yake wanamepanda Mashamba makubwa na sasa wana una na kuipatia nchi hiyo dola milioni 14 kwa Mwaka.

Amesema a nashukuru kwenye Ilani hii mpya ya Chama cha Mapinduzi kimeingiza mpango huo wa kuanzisha kiwanda kikubwa cha miti Dawa hivyo ni muhimu sasa kuanza kufikiria huko ili kujihakikishia miti Dawa ya kutosha kiwanda hicho kitakapoanzishwa.

Mhe. Prof. Kabudi  amefurahi kusikia kwa mara ya kwanza kuwa SUA ndio yenye hospitali pekee ya Taifa ya Rufaa ya Wanyama na kwamba hili Ni jambo kubwa ambalo Watanzania wanapaswa kulijua na hivyo kuitumia kikamilifu.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA amemuonesha Mgeni rasmi Prof. Kabudi matrekta kumi ambayo SUA imepewa na Mhe. Rais Dkt.  John Pombe Magufuli na kusema kuwa yamekuwa chachu ya kuongeza mengine na vifaa mbalimbali vya kulimia na kufundishia kutoka na mapato ya ndani.

No comments: