Nyamhanga aiagiza NHC kukamilisha ujenzi wa nyumba Oktoba


 KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Joseph  Nyamhanga ameligiza Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kuhakikisha kuwa linakamilisha haraka ujenzi wa Machinjio mpya ya Vingunguti ili ianze kutumika kwa majaribio ifikapo mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

Aidha amelipongeza Shirika hilo ambalo ndilo limepewa dhamana ya ujenzi huo kwa hatua za haraka ilizozichukua katika ujenzi wa Machinjio hiyo kutokana na kusuasua hapo awali kabla ya Rais John Magufuli kutoa agizo la kutaja ujenzi huo kukamilika mapema.

Nyamuhanga alitoa agizo hilo jana wakati akikagua ujenzi wa miradi balimbali ya kimkakati iliyopo jijini Dar es Saalam ambapo amesisitiza kuwa kwa ujumla wake miradi hiyo ipatayo 20 nchi mzima inaigharimu Serikali kiasi cha zaidi ya Bilioni  288.

"Pamoja na maendeleo mazuri ya ujenzi, naawagiza NHC ambao ndiye aliyepewa la kuwa mkandarasi wa ujenzi huu, kuhakikisha anakamilisha haraka ujenzi huu ili kutoa fursa ya machinjio kuanza kazi" alisema Nyamuhanga.

Alisema kimsingi  Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha  wanawekeza miradi mingi iwezekanavyo kwa ajili ya kusaidia huduma mbalimbali za wananchi na kusisitiza kuwa ni vyema miradi hiyo ikalindwa ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri alisema mradi wa Machinjio hiyo ya vingunguti umeigharimu Serikali kiasi cha zaidi ya Sh Bilioni 12 utawezesha kuchinjwa kwa ng'ombe zaidi ya 300 kwa siku na kutoa ajira za kudumu zisizopungua 100 na 300 za muda mfupi.

Alisema kukamilika kwake kutaifanya kuwa machinjio yenye viwango vya kimataifa na hivyo kuliwezesha taifa kufanya biashara ya nyama kimataifa na hivyo kuliingizia fedha za kigeni.

Alisema kinachoendelea kwa sasa katika ujenzi wa machinjio hiyo uliofikia wastani wa asilimia tisini, ni ufungaji wa mitambo mbalimbali kuchinjia pamoja na vifaa vingine vinavyohusiana na ujenzi huo.


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati)akiwa katika ziara ya Ujenzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Vingunguti jijini Dar es Salaam.

No comments: