MRISHO GAMBO AMELISIMAMISHA KWA MUDA JIJI LA ARUSHA AKIREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE...WANANANCHI WAMUAHIDI USHINDI
MGOMBEA wa ubunge Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo leo amesimamisha Jiji la Arusha wakati akirejesha fomu ya kugombea ubunge huku wananchi wakiwemo wanachama wa CCM na wasiokuwa wanachama Chama hicho wamejitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea huyo.
Aidha maeneo mbalimbali ya jimbo hilo wananchi wengi walijitokeza kumuunga mkono, huku wakimwambia asihofu kwani wameshajipanga kumpa kura yeye , madiwani pamoja na Rais na kwamba kura watakazo piga kwa kipindi hiki zitakuwa za kihistoria.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu mgombea Jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM Gambo, aliwashukuru wananchi na wanachama wa CCM kwa kumsindikiza kurejesha fomu huku akiyaamini mapenzi waliomuonesha.
Amebainisha awali miaka ya nyumba kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani watu walikuwa wanaogopa kuvaa hata sare za CCM lakini kutokana na kazi alizofanya Rais wetu na zimekubalika ndio maana sasa hivi wanaweza kuvaa sare hizo na kupita sehemu yeyote Ile
Amesema iwapo tume itampitisha atashirikiana nao pamoja na viongozi katika kila jambo ili Kuhakikisha Chama chao kinapita pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo
"Namshukuru Mungu kwa kunisimamia kila hatua maana anapo simama hakuna anaezuia, Mungu akiamua kitu hamna binadamu anaeweza kuzuia.Niwaombe mniombee mimi na Rais wetu,"amesema Gambo
Amesema kuwa alipokuwa njiani anaelekea kurejesha fomu alipokea ujumbe mfupi wa maneno uliotoka kwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA unaosema " Nilikuwa sijui kama wewe ni mjomba wangu ,na iwapo ningejua unapitishwa na Chama chako nisinge gombea .
"Mimi namtumia tu taarifa kuwa mama yangu alikuwa ni mchaga na nimwambie sio mamangu tu hata mke niliyemuoa ni mchaga, kwa hiyo yeye asihofu aje tukutane uwanjani tujue mbivu na mbichi, naniseme tu tukipitishwa naahidi kupiga kampeni za amani na utulivu,"amesema Gambo.
Ameongeza kuwa aao hawatapeleka majungu kwenye majukwaa bali wataenda kuelezea shida za wananchi na kuwaambia namna ya kuzitatua.Amewataka wananchi kundelea kutunza kadi zao za kupiga kura ili ikifika Oktoba 28,2020 wajitokeze wakachague viongozi watakao waongoza vyema.

No comments: