MGOMBEA UBUNGE (CCM) JIMBO LA LUDEWA JOSEPH KAMONGA APOKELEWA KWA KISHINDO MARA BAADA YA KUCHUKUA FOMU
Na Shukrani Kawogo, Njombe.
Mbunge aliyemaliza muda wake Deo Ngalawa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baadhi ya wagombea wa kura za maoni pamoja na wananchi katika kumsindikiza mgombea ubunge aliyeteuliwa na chama hicho Joseph Kamonga kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Ludewa
Akizungumza baada ya zoezi hilo la uchukuaji fomu kukamilika Ngalawa amesema kuwa chama kimepata mgombe sahihi hivyo ameamua kumuunga mkono Kamonga ili kuongeza nguvu ya maendeleo katika Jimbo hilo.
" Nimefurahi kutoka moyoni kwa kuteuliwa Kamonga, na ninauhakika ataendeleza pale nilipoishia mimi na ataweza kufanya zaidi ya niliyoyafanya Mimi", Alisema Ngalawa.
Aidha kwa upande wa Kamonga amemshukuru Ngalawa na kumuahidi kukitendea haki kijiti alichomkabidhi.
Katika zoezi hilo la uchukuaji fomu liliambatana na maandamano ya waendesha pikipiki, magari pamoja na watembea kwa miguu ambao walikuwa sambamba na msafara huo

Baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa wamemnyanyua juu mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa kupitia chama hicho Joseph Kamonga
Mama mzazi wa mgombea ubunge Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akimpongeza kijana wake kwa kuchukua fomu wakiwa katika ofisi ya mkurugenzi wa uchaguzi.
.
Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kulia) akicheza ngoma ya mganda pamoja na wanakindi Cha ngoma hiyo kutoka Ludewa kijijini
Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (katikati) akionyesha fomu ya ugombea ubunge baada ya kuichukua kwa mkurugenzi wa uchaguzi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba na kushoto ni aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Deo ngalawa
Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume(kulia) akizungumza na mgombea ubunge Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga pamoja na wagombea udiwani kata mbalimbali za wilaya hiyo
Kikundi Cha ngoma ya mganda kikitumbiza mbele ya mgombea ubunge wa CCM jimbo la Ludewa Joseph Kamonga pamoja na viongozi mbalimbali ( hawapo pichani)
Mgombea ubunge jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwapungia mkono wananchi ( hawapo pichani) akiwa katika msafara wa kwenda kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo
Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ( kulia) akisaidiana na aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Deo Ngalawa kuhakiki fomu alizokabidhiwa na mkurugenzi wa uchaguzi Sunday Deogratius
Mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Ludewa Sunday Deogratius(Kulia) akimkabidhi fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo hilo Joseph Kamonga.
Baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja na mgombea ubunge Jimbo la Ludewa, kutoka kushoto ni katibu wilaya Bakari Mfaume, katibu UWT ludewa, Katibu umoja wa vijana Baraka, mama mzazi wa mgombea ubunge, aliyekuwa mbunge Deo Ngalawa, mgombea ubunge Joseph Kamonga, mwenyekiti Stanley Kolimba na Mwenyekiti wa umoja wa vijana Theopista Mhagama.
No comments: