MFUKO WA TAIFA BIMA YA AFYA WAJIKITA KUWAFIKIA WANANCHI KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI

Na Pamela Mollel, Arusha

Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya NHIF umejikita katika kuwafikia wananchi wake katika maeneo mbalimbali hapa Nchini

Akizungumza hivi karibu katika maonesho ya nanenane Kanda ya kaskazini Meneja wa mfuko huo Isaya Shekifu amesema kuwa wamejipanga kikamilifu kuwafikia wananchi waliopo mijini na vijijini

Alisema kuwa mfuko huo wa bima unavituo zaidi ya elfu saba 7000 huku Arusha vituo zaidi ya mia tatu hamsini(350)Jambo ambalo limewafanya wananchi waendelee kupata huduma hiyo

Aidha aliongeza kuwa kwa Sasa wameweza kuongeza wigo wa wanachama ambopo kwa wanamakundi zaidi ya sita

Alitaja makundi hayo  kuwa Bima ya waandishi wa habari,Bima ya Umoja hii ni kwaajili ya vikundi mbalimbali vya jasiriamali,Wamachinga,Madereva na Wakulima

Afisa Matelezo wa mfuko huo Miraji Kisile alisema kuwa bado wanaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali juu ya Bima ya Afya,namna ya kuwa na bima,faida zake na hasara za kutokuwa na bima

Pia alisema sambamba na hilo wanatoa elimu ya Afya ambapo baada ya kupima magonjwa yasiyoambukiza yalionekana kuwa changamoto ukilinganisha na yale yanayoambukiza.
 Meneja Mkoa wa Arusha wa bima ya Afya(NHIF) Isaya Shekifu akiongea na waandishi wa habari katika banda lao kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana katika mfuko huo
 Afisa matelezo wa mfuko huo Arusha Miraji Kisile akizungumza na waandishi wa habari
 Maafisa wa mfuko huo wakijadiliana jambo
 Kulia ni Gloria Mziray Afisa wa mfuko huo akiwa anamsikiliza moja ya mwananchi aliyefika katika banda hilo

No comments: