MATUKIO KATIKA PICHA: TUKIO LA MOTO KATIKA KIWANDA CHA BORA, TAZARA JIJINI DAR LEO
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiendelea na zoezi la uzimaji moto uliotokea katika moja ya maghala ya Kiwanda cha kutengeneza kandamili cha Kampuni ya Bora, eneo la Tazara jijini Dar es salaam mchana wa leo. Moto huo ambao chanzo chake hakikuweza kufahamika kwa haraka, uliteketeza moja ya maghala hayo pamoja na gari kubwa (Lori) ambali lilikuwa tayari limesheni mzigo huo kwa kusafirisha mikoani. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi, Bakari Mrisho alisema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo hasa cha moto huo ambao kikosi chake kilifanikiwa kuudhibiti ili usiendelee maeneo mengine.
Zoezi la uzimani moto huo likiendelea kwa ushirikiano mkubwa wa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akiwa katika eneo la tukio akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Jeshi la Zimamoto Uokoaji, wakati alipofika kujionea hali halisi ya tukio hilo la moto, mchana wa leo eneo la Tazara, jijini Dar es salaam.
No comments: