KATIBU MKUU ALAT FAGILIA MIRADI YA MAENDELEO

Mhandisi Majengo Jiji la Mwanza, Tunaye Mahenge (kushoto) akimueleza Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Serikali Mitaa Tanzania (ALAT) Elirehema Kaaya (kulia) changamoto ya mkondo wa maji kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa wodi ya wanaume katika Hospitali ya Nyamagana jana.
Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya (wa pili kulia) akizungumza jambo na wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Iseni B, katikati ni mSalm Hussein Yusuf aliyemweleza Rais John Magufuli changamoto ya upungufu wa madarasa na matundu ya vyoo ambapo zaidi ya wanafunzi 1300 walikuwa wakitumia matundu 9 tu ya vyoo na darasani wakikaa kwa kusongamana.Rais alichangia sh. mioioni 5 za ujenzi wa madarasa.Picha zote na Baltazar Mashaka.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Nsumba, Denis Mwakisimba (kulia) jana akimuongoza Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Serikali Mitaa Tanzania (ALAT) Elirehema Kaaya (kushoto) kukagua miundombinu ya shule hiyo kongwe iliyokarabatiwa kwa sh. milioni 876.9.Shule hiyo ilijengwa mwaka 1962.
Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya, akielekeza jambo wakati akikagua barabara ya Majengo Mapya inayojengwa kwa kiwango cha lami wilayani Nyamagana.

Na Baltazar Mashaka, Mwanza
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Serikali Mitaa Tanzania (ALAT) Elirehema Kaaya, amesema miradi mikubwa ya kimkakati iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa mapato ya ndani kwenye sekta za afya,elimu na miundombinu ya barabara imeleta matokeo chanya na kuakisi maisha ya wananchi 

Kaaya alisema jana wakati akikagua miradi ya maendeleo ya elimu, afya na miundombinu ya barabara iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa fedha za mapato ya ndani, wahisani na serikali kuu.

Alisema miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami, hospitali, vituo vya afya na zahanati, vyumba vya madarasa na ukarabati wa shule kongwe imetekelezwa kwa ubora wa hali ya juu kulingana na thamani ya fedha.

Akiwa katika shule ye msingi Iseni B. Kaaya alishuhudia madarasa mawili yaliyojengwa kwa fedha zilizotolewa na Rais John Magufuli baada ya kuombwa na mwanafunzi Salma Yasin awajengee madarasa wakati wa ziara yake mwaka huu.

“Serikali ya Awamu ya Tano ni ya vitendo, imetenda haki kwa wananchi wake wanyonge kwa kutumia kodi zao kuleta maendeleo na kuhakikisha kero zao zinaondolewa na vilio vyao vinasikika kama ilivyokuwa sauti ya binti Salma Hussein Yasin (mwanafunzi) aliyemwomba Rais John Magufuli kuwajengea miundombinu ya madasara na akatekeleza,”alisema Kaaya na kuongeza;

“ Kongole kwa wanafunzi hasa binti aliyemuomba Rais kuwajengea vyumba vya madasrasa, hili ni jambo jema.Si hayo tu pia serikali imetekeleza miradi ambayo imeleta tija na matokeo chanya kwa wananchi.”

Alisema serikali imetekeleza miradi mikubwa ya afya na elimu ikiwemo elimu bure ambapo imejenga mundombinu ya madarasa na kukrabati shule kongwe zikiwemo shule walizosoama marais wa Awamu ya Kwanza Hayati Baba wa Taifa , Mwl Julius Nyerere na Benjamin Mkapa , wa awamu ya tatu.


Kwa upande wake Salma Yasin alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Magufuli kwa namna alivyopokea ombi lake na kukubali kuwajengea madarasa mawili ambayo yamesaidia kupunguza upungufu wa madarasa na leo wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo wanayatumia.


“Namshukuru sana Rais Magufuli kwa kukubali kutujengea vyumba vinne vya madarasa, Mwenyezi Mungu ambariki leo tuna furaha kusoma tukiwa ndani ya miundombinu bora,”alisema.

Mwanafunzi huyo alimshangaza Katibu Mkuu wa ALAT baada ya kumwuliza baada ya kihitimu anataka kuwa nani ambapo alisema lengo lake baada ya kihitimu elimu yake ni kuwa Makamu wa Rais Mungu akimjalia uhai. 

Naye Mkuu wa shule hiyo ya Iseni B Donald Chakachaka alisema ili kumuezi Rais Magufuli wameweka sanamu ya ndege ikiwa ni nyenzo ya kufundishia lakini pia kukumbuka jinsi alivyorejesha na kuboresha usafiri wa anga kwa kununua ndege 11 ndani ya miaka minne tangu alipoingia madarakani.

“Sanamu hii ya ndege inatumika kufundishia lakini pia ukumbusho wa zaira ya Rais Dk. Magufuli na jitihada zake za kurejesha usafiri wa anga kwa kufufua Shirika la Ndege (ATC) na kununua ndege mpya ili kukuza uchumi kupitia sekta ya usafiri wa nga,”alisema.

Aidha Kaaya aliagiza shule zote za Halmashauri ya Jiji la Mwanza kufanya mikakati ya makusudi kujenga miundombinu ya kuvuna na khifadhi maji ya mvua yatakayotumika kwa usafi, kuotesha miche na kupanda miti ili kuboresha mazingra ya shule.
Alisema wakipanda miti mbali na kutunza mazingira watakuwa wamewajengea wanafunzi stadi za maisha na mazingira hivyo wauone umuhimu huo wa kujenga matenki ya kuhifadhi maji na gatter za kuvuna maji ya mvua.

No comments: