GUNIA 116 ZA BANGI ,MISOKOTO 714 YAKAMATWA ARUMERU

 Kamishana Jenerali James  Wirbert Kaji akizungumza na waandisi wa habari wakati wa zoezi la kuteketeza shehena ya bangi  magunia 116 katika kitongoji cha Karatini Kisimiri chini wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha.Picha zote na Vero Ignatus.
Baadhi ya magunia ya bangi yaliyokamatwa katika operesheni ya kusaka madawa ya kulevya, Kisimiri wilaya Arumeru mkoani Arusha.
Kutoka kushoto ni Kamishana Jenerali James  Wirbert Kaji Mamlaka ya kupambana na Dawa za kulevya, ACP Salum Hamdun,Mkuu wa kikosi cha usalama mkoa wa Arusha Solomon Mwanamilo kwa pamoja wakiwasha moto kuteteteza bangi iliyokamatwa katika operesheni ya kusaka madawa ya kulevya ikiwemo bangi 
Wa pili kutoka kushoto  ni Kamishana Jenerali James  Wirbert Mamlaka ya kupambana na Dawa za kulevya , Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamdun,Mkuu wa kikosi cha usalama mkoa wa Arusha Solimon Mwangamilo wakiwa wanawasha moto tayari kuteketeza dawa hizo za kulevya


Na.Vero Ignatus-Arumeru

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Arusha ,wamekamata dawa za kulevya aina ya bange magunia 116 ,pamoja na watuhumiwa 3 katika kitongoji cha Karatini Kisimiri chini wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha katika operesheni ya biashara haramu ya bangi .

Katika operesheni iliyoongozwa na Kamisha  Jeneral Wirbert Kaji pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa rusha ACP Salum Rashid Hamdun,  pamoja na magunia 116 vilikamatwa viroba tisa(9)vya bangi na misokoto 714 ya bangi.
Mtuhumiwa mmoja Kanael Ndakausi (50)Akyoo mkazi wa Karatini Kismiri chini alikamatwa akiwa nagunia (3) za bangi na viroba ( 9)vya bangi vyote vikiwa vimehifadhiwa ndani ya nyumba yake

Aidha magunia mengine 113 yalikamatwa kwenye nyumba zaidi ya 20 za wakazi wa eneo hilo ambapo watuhumiwa walifanikiwa kukimbia makazi yao kabla ya kukamatwa,ambapo mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamishana Jenerali James  Wirbert Kaji alisema baadhi ya watuhumiwa wamekimbia hivyo dawa hizo za kulevya ambazo hazikuwa na watuhumiwa wameziteketeza 

Aidha Kamisha Kaji alitoa onyo kali huku akisema kuwa Arumeru imekuwa ni tatizo kubwa kwani hivi karibuni waliweza kukamata zaidi ya gunia 140 ambapo wamekamata gunia 116,amewasihi wananchi kwa Tanzania nzima wazidi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwani bangi siyo nzuri na vita hiyo ni vita ya wotena siyo ya mamlaka peke yake . 

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Arusha (ACP)Salum Hamdun amesema Jeshi litaendelea kufanya operesheni katika kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi vya ulinzi na usalama, amesema hata kukamatwa kwa magunia hayo 116 ni matokeo ya ushirikiano baina ya Jeshi la polisi,Mamlaka ya Udhibiti na vyombo vingine vya usalama
Amesema hapo siyo mwisho wataendelea kufanya oparesheni za mara kwa mara japo kuwa bangi hiyo hulimwa milimani na wakati mwingine inakuwa ni vigumu kufika huko lakini jeshi hilo litajitahidi kuhakikisha kwamba kilimo hicho cha bangi kinadhibitiwa .

Ametoa rai kwa watendaji wa serikali katika ngazi vitongoji,vijiji  kutokukaa kimya pale wanapoona viashiria hivyo na kuwataka  kutoa taarifa za mapema kwa kushirikiana na wananchi raia wema, ili kuhakikikisha kwamba kilimo hicho cha bangi kinakoma.

No comments: