Goba Road Runner watoa msaada wa vifaa tiba katika Zahanani ya Goba
Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya akikabidhiwa Vifaa vya afya na Mwenyekiti wa bodi ya Goba Road Runner(GRR), Fritz Msanjo ambavyo ni Barakoa, Grovis, na vifaa ya kusaidia mama kujifungua (suction machines) katika Zahanati ya Goba iliyoko Manispaa ya Ubungo ikiwa ni mchango kwa jamii.
Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya akizungumza na wanachama wa Goba Road Runner(GRR), wauguzi wa zahanati ya Goba wakati wa kukabidhiwa kwa vifaa vya afya kwenye kituo hicho cha afya vilivyotolewa na uongozi wa Goba Road Runner(GRR) ikiwa ni kurudisha mchango kwenye jamii.
Mwenyekiti wa bodi ya Goba Road Runner(GRR) Fritz Msanjo akitolea ufafanuzi baadhi ya kazi zinazofanywa na Goba Road Runner(GRR) hasa kwenye mchezo wa kukimbia pamoja na kushiriki kwenye jamii inayowazunguka wakati wa kukabidi vifaa tiba katika Zahanati ya Goba iliyopo Manispaa ya ubungo jijini Dar es Salaam.
Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya akipeana mkono na Sulleiman Shermax, Mwenyekiti Kamati ya Fedha mara baada ya kulipa pesa ya kuwa mwanachama wa Goba Road Runner(GRR) wakati wa kukabidi vifaa tiba katika Zahanati ya Goba iliyopo Manispaa ya ubungo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Goba Road Runner(GRR), wauguzi na wanasiasa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya wakati wa kukabidhi vifaa tiba katika Zahanati ya Goba iliyopo Manispaa ya Ungungo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Goba Roads Runners(GRR), Revocatus Kahendaguza akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo pamoja na kutambulisha wajumbe wa Goba Roads Runners(GRR) walifika kwenye Zahanati ya Goba kwa ajili ya kutoa msaada wa vifaa tiba kwenye Zahanati hiyo leo.
No comments: