CCM TUNDURU YATAMBA KUFANYA VIZURI KATIKA UCHAGUZI MKUU
Na Mwandishi Wetu, Tunduru
CHAMA CHA MPINDUZI (CCM) Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma kimetamba kupata ushindi wa kishindo katika kinyang'anyiro cha Urais, Ubunge na Madiwani katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tunduru Mustafa Bora amesema hayo jana wakati akiongea na Wagombea walioteuliwa kupeperusha bendera ya Chama hicho katika majimbo ya Tunduru kusini Daimu Iddi Mpakate na Tunduru Kaskazini Hasani Zidadu Kungu baada ya kukabidhiwa Fomu za wagombea Ubunge za Tume ya Taifa ya uchaguzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa wilaya hiyo Gasper Balyomi.
Bora alisema kuwa kupitia Uchaguzi huu Chama cha mapinduzi kiliwapembua kwa weledi na kuwateua wagombea ambao wana uwezo wa kutekeleza ilani ya chama ya mwaka 2020/2025 na kuwaletea maendeleo Wananchi wake bila kujali itikadi ya vyama.
“ Chama cha mapinduzi CCM) kipo imara , kinao wagombea wenye sifa na wanao uzika bila kutia mashaka kutokana na kukubalika kwa wananchi” alisisitiza Bora.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wagombea hao Daimu Iddi Mpakate na hasani Zidadu Kungu pamoja na kuwapongeza Viongozi wa Kamati za Siasa Wilaya,Mkoa na Halmashauri kuu ya Taifa kwa kuwateua walisema kuwa wapo tayali kuwa daraja kati ya wananchi na Serikali katika kuwatumikia wananchi wa majimbo yao.
Wagombea hao walibainisha baadhi ya Vipaumbele vyao kuwa ni pamoja na kusimamia Elimu, Afya ,maji na Miundombinu ya barabara katika maeneo ya majimbo yao.
Awali msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmamshauri ya wilaya ya Tunduru Gasper Balyomi aliwataka wagombea hao kuwa makini katika kusoma na kujaza taarifa zao katika fomu walizo kabidhiwa vinginevyo hawatapatiwa Barua za kuteuliwa kuwania nafasi hizo kupitia chama chao.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tunduru Kitte Mfilinge alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wananchi wa Wilaya hiyo kuwa chama chake kitafanya kampeni za ustaarabu, hakita tumia lugha za matusi dhidi ya wagombea wa vyama vingine.
Aidha,Mfilinge aliwataka wanachama, Wakeleketwa na wananchi kwa ujumla kuwa makini wakati wa kusikiliza Sera zinazo tekelezeka kutoka kwa wagombea makini walioteuliwa na chama chake na kuwaunga mkono kwa kuwapigia kura nyimgi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.
No comments: