BOMBA KUBWA LA INCH 10 KUPELEKA MAJI ENEO LA MBEZI LUIS


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam  (DAWASA) imesema inaendelea jitihada kuhakikisha Maji yanawafikia wananchi kwa wakati katika eneo la Mbezi Luis linalojumuisha maeneo ya Makabe, Uzunguni, Hekima, Mageti, Kwa Robert, eneo la Muhimbili, maeneo ya ukanda wa juu wa Matosa.

Meneja wa DAWASA, Kimara Mhandisi Pascal Fumbuka akizungumza katika eneo hilo wakati wakuweka Miundombinu ya Maji amesema mradi huo unafanywa na Taasisi hiyo ya DAWASA kuhakikisha Wananchi wote wa jiji la Dar es Salaam wanapata huduma ya maji ya uhakika.

Amesema jumla ya Kilometa 2.3 zimelazwa chini kwenye eneo hilo kuhakikisha upatikanaji wa maji hayo, amesema matarajio kukamilisha mradi huo August 20 kufungulia maji na kuwafikia wananchi wa ukanda huo wa Mbezi na kuondoa Bomba la Inchi Nne ambalo limeziwa katika upande huo.

Amewashukuru wananchi kwa uvumilivu, amesema jitihada zinaendelea na wananchi huo watapata huduma hiyo kwa wakati uliopangwa na Mamlaka hiyo ya DAWASA.
Meneja wa DAWASA Mkoa wa Ubungo, Mhandisi Pascal Fumbuka akijadilina jambo na wafanyakazi  wa mamlaka hiyo wakati wa kuweka bomba litakaloweza kisambaza maji katika eneo la Mbezi Luis linalojumuisha maeneo ya Makabe, Uzunguni, Hekima, Mageti, Kwa Robert, eneo la Muhimbili, maeneo ya ukanda wa juu wa Matosa.
Tingatinga likiwa limebeba bomba la DAWASA kwalitakaloweza kuhudumia katika eneo la Mbezi Luis linalojumuisha maeneo ya Makabe, Uzunguni, Hekima, Mageti, Kwa Robert, eneo la Muhimbili, maeneo ya ukanda wa juu wa Matosa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA, Neli Msuya akipata maelezo kutoka kwa  Meneja wa DAWASA Mkoa wa Ubungo, Mhandisi Pascal Fumbuka kuhusu mradi wa maji eneo la Mbezi Luis linalojumuisha maeneo ya Makabe, Uzunguni, Hekima, Mageti, Kwa Robert, eneo la Muhimbili, maeneo ya ukanda wa juu wa Matosa.


Meneja wa DAWASA Mkoa wa Ubungo, Mhandisi Pascal Fumbuka akionesha chanzo cha maji lililounganishwa kutoka kwenye bomba kubwa yatakayosambazwa katika maeneo mbalimbali ya Kimara pamoja na Mbezi 
Muonekano wa bomba la maji lililounganishwa kutoka katika bomba kubwa kwa ajili ya kuhudumia wakazi wa eneo la Mbezi Luis linalojumuisha maeneo ya Makabe, Uzunguni, Hekima, Mageti, Kwa Robert, eneo la Muhimbili, maeneo ya ukanda wa juu wa Matosa.
Meneja wa DAWASA Mkoa wa Ubungo, Mhandisi Pascal Fumbuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa maji utakaowahudumia wakazi wa  eneo la Mbezi Luis linalojumuisha maeneo ya Makabe, Uzunguni, Hekima, Mageti, Kwa Robert, eneo la Muhimbili, maeneo ya ukanda wa juu wa Matosa.

No comments: