VIWANDA 16 VYA DAWA,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI VINAJENGWA NCHINI-FIMBO
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo amesema katika kwenda na dhamira ya kuwa nchi ya viwanda,TMDA kwa kuhamasisha wadau tayari viwanda 16 vimeanzishwa na viko katika hatua mbalimbali ya kuanza kuzalisha dawa,vifaa tiba pamoja na vitendanishi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) baada ya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika katika udhibiti wa wa Dawa , Vifaa Tiba na Vitendanishi kwa kufikia ngazi ya tatu kati ya nne za udhibiti wa dawa kupitia Mamlaka hiyo.
Fimbo amesema kuwa wamekuwa karibu na wadau wanaoanzisha viwanda vya uzalishaji wa dawa,Vifaa tiba pamoja na vitendanishi wanaratibu kwa kila hatua.
Fimbo aliyasema hayo wakati akizungumza katika kikao kazi cha Uhamasishaji wa Waandishi wa habari kuhusu usimamizi wa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba kutoka Mikoa ya Morogoro,Dar es Salaam na Pwani kilichofanyika mkoani Morogoro na kusisitiza lengo ni kufikia hatua malengo katika utoaji wa huduma.u
Amesema kuwa hatua ya mafanikio hayo inayotambuliwa na WHO ilifikiwa mwaka 2018 na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi za mifano Dunia huku nchi mbalimbali zikija kujifumza mafanikio hayozikiwemo Uganda,Rwanda,Zambia,Sudan na Botswana na nyingine kutoka nchi za Ulaya.
Naye Meneja wa Huduma za Sheria,Iskari Fute,akijibu maswali ya Waandishi wa habari baada ya kuwasilisha mada ya sheria ,Muundo na Wigo wa Sheria ya TMDA,alisema wamefanikiwa kuwabaini watuhumiwa 147 hapa nchini wanaokiuka sheria za mamlaka hizo ambao kati yao 32 wametozwa faini na wengine 32 kesi zao bado zinaendelea mahakamani huku 82 wakiendelea na uchunguzi katika vituo mbalimbali hapa nchini katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Amesema watuhumiwa 32 mpaka sasa wameshakiri makosa yao na kulipa faini jumla ya shilingi milioni tano huku wakihaidi kufuata sheria za mamlaka hiyo.
Amesema kuwa watuhumiwa hao walibainika baada ya TMDA kufanya kaguzi mbalimbali za kushtukiza katika maeneo tofauti ikiwa ni lengo la mamlaka katika kulinda afya ya jamii ili sheria ya Dawa na Vifaa Tiba sura ya 219 iweze kufuatwa.
Kwa upande wake akifungua kikao kazi hicho,Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Morogoro,Anza Ndossa,aliwataka waandishi wa habari nchini kuhakikisha wanatoa mchango wao kuisaidia TMDA ili iweze kufikia malengo yake ya kutoa huduma bora.
Hata hivyo aliwatahadharisha wafanyabiashara wanaojihusisha na Usambazaji wa Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi kufuata taratibu na sheria zilizowekwa kutokana na uwepo wa wimbi kubwa la watu wanaoendesha shughuli hizo mitaani bila kuwa na kibali toka TMDA.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Morogoro,Anza Ndossa akizungumza wakati akifungua mkutano wa wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA uliofanyika mkoani humo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA,Adam Fimbo akizungumza na waandishi katika mkutano wa kuwajengea uwezo uliofanyika mkoani Morogoro.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano wa kuwajengea uwezo uliofanyika mkoani Morogoro.
Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA Gaudensia Semwanza akitoa maelezo katika mkutano wa waandishi uliofanyika mkoani Morogoro
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo uliofanyika mkoani Morogoro(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Picha ya pamoja
No comments: