TRC YAANDA MPANGO WA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI WALIOTHIRIWA NA UJENZI WA RELI YA KISASA

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Amina Lumuli akizungumza na wadau mbalimbali kuhusiana na mpango wa shirika hilo kuboresha maisha wananchi waliothiriwa na ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Meneja Uhusiano wa TRC Jamila Mbarouk akitoa maelezo katika mkutano wadau kuhusiana na mpango wa kuboresha maisha kwa wananchi walioathiriwa na ujenzi wa Reli ya Kisasa.
 Mkurugenzi wa Huduma ya Simu kwa Mtoto wa Shirika la C-Cema  Michael Marwa akizungumza namna shirika hilo linavyofanya kazi katika masuala ya ukatili kwa watoto.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa wa SIDO Stephen Bondo akitoa  uzoefu wa SIDO katika utoaji wa elimu ya ujasiriamali na namna watavyoshiriki kwa wananchi katika mpango wa TRC.
 Wadau wakifatilia hotuba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC Katika ulioandaliwa kuhusiana na mpango kuboresha maisha kwa wananchi walioathiriwa na mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC Amina Lumuli (katikati) wakisaini  makubaliano  na Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Profesa Sylivester Mpanduji  wa tatu kutoka kushoto makubaliano hayo yamefanyika katika mkutano wa wadau uliondaliwa na TRC.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC Amina Lumuli akibadilishana hati na mkurugenzi Mkuu wa SIDO Profesa Sylivester Mpanduji.

*Yashirikisha wadau mbalimbali wa kutekeleza  mpango huo.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limekutana na wadau kutoka Taasisi za Serikali pamoja mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuweza kushirikiana na katika utoaji wa elimu kwa wananchi waliothiriwa  na mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) katika mpango wa kuboresha maisha.

Shirika hilo limeandaa mpango ya kusaidia wananchi walipitiwa na mradi huo kwani kuna wengine wametwaliwa ardhi yao kwa kuondoka katika maeneo yao huku wengine biashara hivyo kunahitajika kuwajenga katika kurudi katika maisha walioyazoea.

Akizungumza na wadau hao Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo  Amina Lumuli amesema  mpango huo ni pamoja na kuanzisha shughuli za ujasiriamali itakayofanywa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) pamoja na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kutoa elimu kwa wananchi waliopitiwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge.

Lumuli amesema kuwa katika ujenzi huo kuanzisha mpango huo ni kutaka wananchi hao kuona huo mradi haujaathiri  maisha yao kutokana  na kuwepo kwa mpango ni  kuhakikisha  wananchi walioko kandokando ya reli wananufaika na fursa mbalimbali.

Amesema moja ya jitihada ambazo zimefanyika ni pamoja na kulipa fidia kwa wale waliotwaliwa ardhi,nyumba yao  katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kuzinagatia viwango vilivyowekwa kamataifa.

Lumuli amesema wadau hao watatumika katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi kwa kutumia utaalam wao wa kufanya waelewe malengo ya serikali kujenga reli ya kisasa ambayo ni ya watanzania

 Mkutano huo ulikwenda sambasamba na kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango huo kwa baadhi ya wadau ikiwa na lengo wadau wanawafikia wananchi  walioathiriwa na ujenzi wa reli ya kisasa.

Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa wa SIDO Stephen Bondo amesema kuwa SIDO imekuwa ikitoa mafunzo kwa kwa wajasiriamali na kumekuwa na mafanikio hivyo hata hao walipitiwa na mradi wa reli ya kisasa watanufaika.

Mkurugenzi wa  Huduma ya Simu kwa Mtoto wa Shirika  la C-Sema Michael Marwa amesema kuwa katika ujenzi huo ni kuangalia masuala ya ukatili wa kwa watoto ikiwa ni pamoja na kutoa elimu katika eneo hilo.

No comments: