TIA yatoa mafunzo kwa Wahasibu na Wakaguzi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akizungumza wakati akifungua mafunzo Wahasibu na Wakaguzi wa Wizara hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu-Taasisi Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknoloojia  Sebastian Inoshi akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo ya wahasibu na wakaguzi wa Wizara hiyo.
 Mshauri Mwelekezi na Mratibu wa Mafunzo wa TIA Dkt.Hasanal Isaya  akitoa maelezo kuhusiana na wanavyotoa mafunzo katika suala la usimamizi wa fedha.
 Mwakilishi wa Mkuu wa  Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Baraka Kamwele akizungumza namna wanavyotoa mafunzo kwa wataalam wa  uhasibu na ukaguzi.
 Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Anna Mhere akizungumza kuhusiana na mafunzo hayo na namna yatavyoleta matokeo chanya.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo.
 Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  akiwa katika picha ya pamoja Wakaguzi wa Wizara hiyo.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James akiwa na Sekretarienti na wawezeshaji wa TIA.

*Profesa Mdoe ataka mafunzo yalete matokeo chanya.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
 WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kuwa mafunzo yanayotolewa kwa wahasibu na wakaguzi yanatakiwa kuleta matokeo ya ufanisi katika kutatua changamoto mbalimbali.

Akizungumza katika mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Wizara hiyo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amesema kuwa mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yanatakiwa kuleta matokeo katika wizara.

Amesema TIA ni wabobezi hivyo fedha ya serikali isiende bure kwani kinchofundishwa kinatakiwa kuleta matokeo na bila kufanya hivyo  hakuna sababu ya kutumia fedha ya serikali katika mafunzo.

Profesa Mdoe amesema mafunzo hayo yatapunguza au kuondoa hoja za ukaguzi katika wizara kwa kuendelea na hati safi inayotokana na utaalam wenu pamoja na mafunzo yanayotolewa.

Amesema kuwa fedha inayotolewa na serikali katika bajeti au fedha inayotoka vyanzo vya ndani  zinatakiwa kusimamiwa katika mipango iliyokusudiawa.

"Mafunzo haya yanayofanyika yanalenga kuimarisha usimamizi wa fedha  hivyo ushiriki wenu wataalam katika masuala haya yatafanya wizara kuendelea kuwa na hati safi"amesema Profesa Mdoe.

Aidha amesema kuwa wakati mwingine inatokea tatizo la ukaguzi ambalo mkaguzi wa ndani hajaona lakini mkaguzi wa nje analiona hivyo mkaguzi wa ndani lazima aweze kungamua hoja za ukaguzi ambapo hadi mkaguzi wa nje  akute hakuna hoja.

Mwakilishi wa Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Baraka Kamwele  amesema kuwa mafunzo haya yamefanyika katika makundi mbalimbali katika kuwajengea uwezo zaidi wakaguzi na wahasibu.

Amesema kuwa kuwa kuna vitu vinabadilika licha kusoma katika maeneo mbalimbali.

Mshauri Mwelekezi na Mratibu wa Mafunzo wa TIA Dkt. Hasanal Isaya amesema katika mafunzo hayo yatatolewa watalaam mbalimbali wakiwemo Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika eneo la utakatishaji.
Amesema kuwa mafunzo hayo ni kuwaongezea ujuzi katika usimamizi wa fedha katika maeneo yao kwa kuwa karibu kati ya wahasibu na wakaguzi wa ndani.

Kwa upande wa Mkaguzi wa Ndani Mkuu Anna Mhere amesema kuwa mafunzo wanayoyapata kwa siku tano yataleta ufanisi kwa wahasibu na wakaguzi .

Mhere amesema kuwa mafunzo yanaumhimu sana kwa watumishi kwa vitu vinabadilika kila siku ambapo Wizara imeweza kuandaa mafunzo katika kada mbalimbali ikiwa ni kutaka ufanisi kwa watumishi katika maeneo yao.

No comments: