TBS WAFIKISHA MAFUNZO WEZESHI KWA WAJASIRIAMALI MKOANI GEITA

Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv.

Semina Maalum Wezeshi kwa Wajasiriamali kufikia matakwa ya Viwango inayoratibiwa na Shirika la Viwango Nchini TBS imewafikia wajasiriamali wa Mkoa wa Geita na kuhudhuriwa na Washiriki ambao ni sehemu ya Wajasiriamali Mkoani humo.

Semina hiyo ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo mengine yaliyowahi kutolewa mapema mwaka huu, Ina lengo la kuwafanya Wazalishaji wa bidhaa hasa wajasiriamali wadogo, kujiinua na kufikia Matakwa ya Viwango ikiwa ni pamoja na namna gani bidhaa zao zitakubalika katika soko la ushindani.

Mgeni Rasmi katika Semina ya Mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Geita Ndg. Fadhili Mohammed amewasisitiza wajasiriamali hao kuongeza ubora wa bidhaa wanazozalisha, ili kuinua kipato chao jambo ambalo litawafanya wajasiriamali hao kujiinua kiuchumi mtu mmoja mmoja na Taifa kwa kwa ujumla, na kwamba Geita ya sasa tofauti na Mikoa mingine inatakiwa kusifika kupitia uzalishaji wa bidhaa zinazokidhi Viwango.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita, Fadhil Mohammed akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Mafunzo Maalum Wezeshi ya Wajasiriamali kufikia Matakwa ya Viwango Mkoani Geita Mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo katika Ukumbi wa SIDO.
Meneja Mafunzo na Utafiti kutoka TBS, Hamisi Sudi Mwanasala akisoma hotuba mbele ya Mgeni Rasmi na Washiriki wa Semina ya Mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu TBS.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Fadhili Mohammed akisikiliza maelezo ya namna bidhaa ya Mafuta inavyotengenezwa kutoka kwa miongoni mwa wajasiriamali walioshiriki Semina ya Mafunzo Wezeshi.
Baadhi ya Washiriki Mkoani Geita  wakiwa wamesimama na bidhaa zao wanazozalisha tayari kwa kumuonesha Mkuu wa Wilaya Geita Ndg. Fadhil Mohammed ( hayupo pichani) aliyefika katika Semina ya Mafunzo Wezeshi kwa Wajasiriamali hao.

No comments: