SIMBA YAFANYA MAZOEZI YA MWISHO KUELEKEA SUMBAWANGA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kabla ya kuanza safari ya kuelekea Sumbawanga katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam 

Simba itacheza na Namungo katika mchezo huo wa fainali siku ya  jumapili kwenye Uwanja wa Nelson Mandela.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani kwa pande zote mbili, Namungo ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa fainali baada ya kupanda ligi Kuu msimu wa 2019/20 huku Simba wakicheza fainali yao ya pili.

Katika mchezo huo utakaochezwa na waamuzi sita, Abubakari Mturo wa Arusha, Abdallah Mwinyimkuu wa Singida, Ahmed Arajiga kutoka Manyara, Ramadhan Kayoko wa Dar, Abdulaziz Ally wa Arusha na Hamdan Said wa Arusha.



No comments: