Waziri wa Maliasili na Utalii atembelea Makumbusho ya Taifa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt Hamis Kigwangala akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga alipotembelea Makumbusho ya Taifa leo
Waziri wa Maliasili na Utalii akitembea katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa kulia kwake ni Balozi wa Finland nchini Tanzania Mhe. Riitta Swan, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Achiles Bufure na nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala akifurahia magari ya historia alipotembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akipimwa joto wakati alipoingia Makumbusho ya Taifa. Wanaotazama ni Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe Riitta Swan na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Dkt. Hamis Kigwangalla akitakasa mikono yake mara baada ya kuingia Makumbusho ya Taifa na kushuhudia hatua zote za usalama dhidi ya ugonjwa wa corona zikifuatwa na kujihakikishia kuwa Makumbusho ni Salama.

No comments: